Upepo mwanana bado unaendelea kumpuliza, staa namba moja wa Bongo
Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ baada ya mgombea anayewakilisha
Muungano wa Vyama vya Upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Omolo Odinga,
kudaiwa kumuita nchini humo.
Kwa mujibu wa chanzo kisicho na chembe ya
shaka, Kiba anayesumbua kwa sasa na wimbo wake wa Seduce Me, alipata
mwaliko huo mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni saa chache mara baada
ya Odinga kushinda kesi ya uchaguzi Katika Mahakama ya Juu aliyokuwa
amemfungulia Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ambaye mambo yalimuwia
mazito.
Kenyatta alitangazwa mshindi wa nafasi ya urais na Tume ya Uchaguzi
na Mipaka ya Kenya (IBEC) katika uchaguzi uliofanyika nchini humo Agosti
8, mwaka huu ambapo Odinga alifungua kesi hiyo mahakamani. Baada ya
mahakama kupitia hoja za pande zote, iliufuta uchaguzi huo kwa kueleza
kuwa tume ya uchaguzi haikuzingatia uadilifu.

0 Comments