Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipuli, Kata
ya Mahina; Rajabu Jumanne (mwenye shati la bluu) akishuhudia zoezi la upimaji
linavyoendelea katika Mtaa wake, likiongozwa na Mratibu/ Mpima; Yohana
Cleophace wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza
wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo Ukuta unaoonekana pichani unategemewa
kuondolewa kupisha utengenezwaji wa barabara za Mitaa.
![]() |
Wataalam wa Upimaji/ Wapima kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la upimaji - Mahina, ambapo beckon zimekuwa zikiwekwa katika viwanja. |
Muonekano wa Barabara iliyochongwa rasmi na Wataalam wa Upimaji/ Wapima
kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la Urasimishaji
katika kata ya Ipuli, Mahina.

Muonekano wa Ramani ya Upagwaji wa Kata ya Mahina - Mwanza

Muonekano wa Ramani ya Upagwaji wa Kata ya Mahina - Mwanza
Muonekano wa Halmashauri ya
Jiji la Mwanza, Ofisi inayohusika kwa karibu zaidi kwa kutumia watumishi wake
wa Mipango Miji kushirikiana na Wananchi katika kurasimisha Makazi holela.
Jiji la Mwanza limepima viwanja
24,000. Ikiwa ni utekelezaji wa dhana ya kuondokana na Makazi Holela katika
Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Akizungumzia mafanikio hayo hivi
karibuni; Mratibu wa masuala ya Urasimishaji, jijini Mwanza, ambaye ni Afisa
Mipango Miji; Athuman. S. Simba alisema; “Katika kufanikisha utekelezaji
uliofanyika; Halmashauri ya Jiji iliunda vikosi kazi vipatavyo kumi na tatu
(13) na kuvipangia majukumu mbalimbali. Vikosi kazi hivyo vilifanya kazi za
uandaaji wa michoro ya mipangomiji, upimaji, ukaguzi wa viwanja na kumilikisha”
Aidha, Katika zoezi zima la upimaji wa
viwanja 24,000. Taarifa yake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza; Hosiana B.
Kusiga; imesema kuwa; Viwanja 19417 vimepimwa (Approved), maeneo ya Kata za
Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, na Nyegezi.
Vile vile, Viwanja 5515 vimefanyiwa
upimaji wa awali (Dermation). Kazi ya upimaji inaendelea katika kata za
Butimba, Mahina, Mkolani, Lwahnima, Igoma, Mhandu, Kishiri na Luchelele. Ambapo Idadi ya viwanja vilivyokamilika na
vilivyo kwenye upimaji wa awali (demarcation) jumla yake ni 25,032.
Utekelezaji wa upimaji huu ni kutoka
kwa agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mhe. William Lukuvi,
kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kuandaa Hati Miliki za viwanja 35,000
kupitia mradi wa urasimishaji makazi holela .
Na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment