Random Posts

Lionel Messi atupia magoli manne Barcelona

 Lionel Messi amefikisha magoli tisa katika msimu huu, na ndio kwanza tupo mwezi Septemba, baada ya kufunga magoli manne wakati Barcelona ikiichakaza Eibar kwa magoli 6-1.

Hii ilikuwa ni hat-trick yake ya pili katika msimu huu, na goli lake la nne ni la 300 kuifungia Barcelona tangu ahamie timu hiyo. Kwa ushindi huo Barcelona inaongoza La Liga kwa tofauti ya pointi tano.
 Leonel Messi akifunga goli la kwanza kwa mkwaju wa penati 
Kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho akifunga goli la pili la Barcelona kwa mpira wa kichwa. 

Post a Comment

0 Comments