Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Moyo Tanzania (THF) katika
kuadhimisha siku ya Moyo Duniani watafanya upimaji wa magonjwa ya Moyo bila
malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa jirani. Upimaji huo utaenda
sambamba na utoaji wa elimu ya lishe
bora kwa afya bora ya Moyo.
Upimaji huu utafanyika katika
viwanja vya Taasisi ya Moyo ambapo wananchi watapimwa urefu, uzito, shinikizo la
damu (BP), sukari na kupewa ushauri. Kwa
wale watakaokutwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa
matibabu. Kauli mbiu ya siku hii ni: “Moyo wenye Afya”.
Katika wiki hii ya maadhimisho ya
Siku ya Moyo Duniani tuna kambi maalum ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua ambayo imeanza
tarehe 25/09/2017 hadi tarehe
29/09/2017. Kambi hii tunaifanya kwa kushirikiana na Taasisi ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani.
Hadi sasa tayari tumewafanyia
upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab (kwa jila la kitaalam Cathertarization) wagonjwa 23, siku ya
kesho tutamalizia kuwafanyia upasuaji wagonjwa watano ili kufiokia idadi ya wagonjwa
28 tuliyolenga. Nia ya kambi hii ni kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa na
kubadilishana uzoefu wa kazi.
Wafanyakazi wa Taasisi hii tunahakikisha
tunatoa huduma bora zaidi za magonjwa ya
moyo kwa wananchi wenye matatizo hayo. Mpango wetu ni kutoa tiba ya moyo, upasuaji wa moyo na elimu kwa jamii ambayo
itawasaidia wananchi kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na magonjwa ya moyo
ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata
ushauri wa kitaalam.
Tangu mwaka 2015 tumewafanyia
upasuaji wa kupasua kifua, kuziba mishipa ya moyo, upasuaji wa mishipa ya moyo,
upasuaji wa mishipa ya damu, kuweka vyuma ndani ya moyo, na kuweka kifaa maalum cha kuusaidia moyo ili
uweze kufanya kazi vizuri (Pacemaker) zaidi ya wagonjwa 1500.
Hatua hiyo imewezesha Serikali kuokoa
zaidi ya shilingi bilioni 45 fedha ambazo zingetumika kuwatibia wagonjwa wa
moyo iwapo wangepelekwa njje ya nchi, hii ni sawa na asilimioa 85.
Taasisi pia
inatoa huduma ya uchunguzi wa kipimo cha magonjwa ya moyo kwa watoto wachanga
waliopo tumboni mwa mama zao (FETAL ECHOCARDIOGRAPHY) ili kujuwa kama
wanamatatizo ya moyo au la.
Tangu kuanza
kutolewa kwa huduma hii mwezi wan ne mwaka huu jumla ya kinamama wajawazito 37 wameshafanyiwa
uchunguzi wa kipimo hicho kati ya hao watoto watano walikutwa na
matatizo ya moyo jambo ambalo litawawezesha
kupata matibabu mapema pindi watakapozaliwa.
Tunawaomba wananchi waadhimishe
siku hii kwa kujitokeza kwa wingi kupima
afya zao hii itawasaidia kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na hivyo kuanza
matibabu mapema kwani asilimia kubwa ya wagonjwa tunaowapokea mioyo yao huo
haiku katika hali nzuri.
Imetolewa na :
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
28/09/2017

0 Comments