Mhe. Ali Kirunda Kivejinja Naibu Waziri Mkuu
ambaye ni Waziri wa Wazira ya Mambo ya
Afrika Mashariki Nchini Uganda, pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki akifungua kongamano la Tamasha la Utamaduni na
Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) leo katika hoteli ya Africana
jiijini Kampala nchini Uganda, aliwasisitiza Wanajumuiya ya Afrika Mashariki kwamba madiliko ya uchumi wa Afrika
yataletwa na Waafrika wenyewe kwa kupitia sanaa na utamaduni wao.
Waliokaa mstari wa mbele ni baadhi ya Washiriki wa Tanzania JAMAFESTI waliohudhuria
uzinduzi wa Kongamano la JAMAFEST lenye kauli mbiu ya " Utamaduni na
ubunifu wa viwanda ni injini ya umoja na kutengeneza ajira".
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel aliyevaa skafu
yenye rangi za bendera ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, akisikiliza kwa
makini maelezo ya ufunguzi wa Kongamano la JAMAFEST.
Baadhi ya Wajasiriamali na Wasanii wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania wakicheza ngoma ya sindimba katika Uwanja Uhuru wa
Kololo ambapo yanafanyika maonesho ya bidhaa za utamaduni na sanaa.
Baadhi ya wajasiriamali wa bidhaa za ubunifu wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania walipopiga picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa
Elisante Ole Gabriel (katikati) mara baada ya uzinduzi wa JAMAFEST jana.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Uganda
Mhe. Dkt. Ruhakana Rugunda akifungua Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya
ya Afrika Mashariki JAMAFEST jana katika Uwanja wa Uhuru Kololo.
Alizihimiza nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuendeleza Matamasha kama JAMAFEST ambayo hutumia mara kwa mara utamaduni
kama njia ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo katika jamii.
Wananchi wa Uganda wakishirkiania na wananchi
kutoka nchi nyingine za Jumuiya za Afrika Mashariki walioshiriki katika
ufunguzi wa JAMAFEST jana.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Uganda Mhe. Dkt.
Ruhakana Rugunda aliyevaa shati la kitenge pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole
Gabriel aliyevaa shati jeupe na skafu ya bendera ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania wakitembea katika Uwanja wa Uhuru Kololo jana kabla ya kufungua
Tamasha la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST.
Mshauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi ambaye pia mwimbaji nguli wa taarab Zanzibar Mhe. Chimbeni Kheri
akiwatumbuiza Wanajumuiya ya Afrika Mashariki walifika katika ufunguzi wa
JAMAFEST katika vuwanja wa Uhuru wa Kololo Kampala nchini Uganda jana jioni.









0 Comments