Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo kuu akisaini
jana kitabu cha wageni mara
alipotembelea ofisi ya Mkuu wa
Wilaya ya Mkuranga ikiwa lengo la ziara hiyo ni kujadili mikakati ya kuzuia wavamizi
kwenye msitu wa hifadhi.
Mkuu
wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga
akimuonesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) Prof. Dos Santos Silayo baadhi ya maeneo ya Hifadhi yaliyovamiwa na kuanzishwa shughuli za
kibinadamu katika Hifadhi ya Msitu wa Vikindu. Lengo la ziara Mtendaji
Mkuu wa TFS hiyo ilikuwa ni kuimarisha
uhifadhi kwa kujadili mikakati ya kuzuia wavamizi kwenye msitu wa
hifadhi.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akiteta neno na
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga wakati wa ziara ya kujionea jinsi wananchi
walivyovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Msitu
wa Vikindu.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo alimpomtembelea
jana Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,
Filberto Sanga ofisini kwake akimuonesha
baadhi ya maeneo kwenye ramani jinsi vyanzo
vya maji vilivyoharibika kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi
kuvamia kwa kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Misitu.
Mwingine ni Meneja Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania wa Wilaya ya Mkuranga Christina Mohamed .
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga mpaka kati kijiji na Msitu wa Hifadhi ya Vikindu mara baada ya kufanya ziara ya kujionea jinsi wananchi walivyovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu katika Hifadhi za Msitu huo.






0 Comments