Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Anastazia Wambura (wa
pili kushoto) na Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia
Ackson wakibeba nyoka anyetumiwa kwa kucheza ngoma ya Bogobogobo kutoka Bujora
Mwanza.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Anastazia Wambura akiongea na wananchi na wanamichezo (hawapo pichani)
waliokuwa wanashiriki Tamasha la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisis ya
Tulia Trust mjini Tukuyu
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Anastazia Wambura akikagua uwanja wa Machinga uliopo mjini Tukuyu ambao
umebadilishwa matumizi na Halmashauri ya Rungwe kwa kukosa sifa w badala yake
uwanja wa michezo sasa utakuwa unatumika ule wa Tandale mjini humo.
Na Eleuteri Mangi,
Tukuyu, Mbeya.
Halmashauri ya Rungwe
imebadilisha matumizi ya uwanja wa zamani wa mpira wa miguu uliopo mjini Tukuyu
unaojulikana kama machinga kuendelea kutumika kwa matumizi mengine kutokana na
kukosa sifa za uwanja huo kukosa sifa.
Badala yake
Halmashauri hiyo imetoa uwanja wa Tandale uliopo mjini Tukuyu kutumika kwa michezo
mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na matamasha mbalimbali.
Hayo yamesemwa na
Mkuu wa wilaya ya Tukuyu Bw. Julius Chalya alipokuwa akitoa taarifa fupi ya
shughuli za maendeleo katika wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani
Mbeya.
“Uwanja wa mwanzo
unaojulikana kama uwanja wa Machinga uliokuwa unatumika kwa michezo kwa sasa haufai
kwa matumizi ya michezo kwa kukosa sifa, hivyo halmashauri imebadilisha
matumizi yake ili uendelee kutumika kwa matumizi mengine ikiwemo kituo cha
mabasi yanayotoa huduma katika halmashauri na bishashara nyingine” alisema Mkuu
huyo wa Wilaya.
Akizungumzia kuhusu
uamuzi wa halmashauri wa kubadilisha matumizi ya uwanja huo wakati wa kufunga
Tamasha la pili la Ngoma za Asili linaloendeshwa na Taasisi ya Tulia Trust,
Naibu Waziri Wambura amesema kuwa Serikali inaendelea kusisitiza halmashauri
ziendelee kutenga maeneo yanayofaa kwa michezo kwa kutimiza vigezo
vinavyotakiwa kwa ajili ya michezo.
Uwanja wa Tukuyu uliokuwa
unatumika zamani kwa michezo umekosa vigezo vya kuendelea kutumika kama uwanja
wa michezo kutokana na vipimo vyake kuonesha kuwa ni mdogo kwa kiwango cha
halisi unatakiwa kuwa na urefu wa mita 68 na huo wa Tukuyu una mita 44.
Kuhusu kuendeleza
kiwanja cha Tandale ambao umetolewa na halmashauri kwa ajili ya michezo, Naibu
Waziri Wambura ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Katibu
Mtendaji wake Mohamed Kiganja kushirikiana na halmashauri hiyo kwa kutoa
ushauri wa kitaalamu kuendeleza uwanja huo ili wananchi wa Rungwe waweze kuutumia
kuboresha afya zao kwa kufanya mazoezi pamoja kunufaika na fursa za kiuchumi
wakati wa mashindano mbalilmbali yatakayofanyika uwanjani hapo.
Kupatikana kwa uwanja
wa Tandale utnaotumika kwa sasa kwa michezo mbalimbali mjini Tukuyu kumepokelwa
na kwa furaha na wananchi waliofurika viwanja hivyo wakati wa kuhitimisha
Tamamsha la pili la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trust
ambapo mwasisi wake Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza
kampeni ya kuirudisha timu ya Tukuyu Stars kwa kuwahamasisha Wabunge wa mkoa wa
Mbeya na wananchi kuiwezesha timu hiyo
kurudi Ligi Kuu ya Tanzania ya Vodacom.




0 Comments