Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha
wadau wa sekta habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio
na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni kilichofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifafanua jambo wakati wa kikao
cha wadau wa sekta habari ili kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika
redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Utangazaji kutoka TCRA, Fred Ntobi, Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Rodney Thadeus.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari(MAELEZO)
Rodney Thadeus akielezea jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya habari ili
kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni
za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada kuhusu kanuni
za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui
mtandaoni wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni hizo
leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria Mwandamizi kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Phillip Filikunjombe akiwasilisha mada kuhusu
kanuni za maudhui ya utangazaji wa na mitandao wakati wa kikao cha wadau wa
sekta ya utangazaji na mitandao ili kujadili kanuni hizo leo Jijini Dar es
Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Evodi Kyando akitoa maelezo kuhusu kanuni
za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui
mtandaoni wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya utangazaji na mitandao ili
kujadili kanuni hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katika) akifuatilia majadiliano ya
wawakilishi kutoka vyombo vya habari vya elekroniki na mitandao wakati wa kikao
cha kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni
za maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba.
Mmoja wa washiriki wa kikao cha wadau wa
utangazaji na waendeshaji wa mitandao Maria Sarungi Tsese (katikati) akichangia hoja
wakati wa kikao cha kujadili kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na
televisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (waliokaa katika) akiwa katika picha ya
pamoja na wawakilishi wa Televisheni na Redio mara baada ya kikao cha kujadili
kanuni za maudhui ya utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za
maudhui mtandaoni leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania Mhandisi. James Kilaba alipowasili kwa ajili ya
kukutana na wadau wa sekta ya habari ili kujadili kanuni za maudhui ya
utangazaji katika redio na tevelisheni, na kanuni za maudhui mtandaoni leo
Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Picha na: Frank Shija
- MAELEZO
.......
Na Pascal Dotto,
MAELEZO
Serikali
imesema kasi kubwa ya maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo
imeikumba sekta ya habari inalazimu jamii kufanya maboresho ya mara kwa mara ya
Sera na Kanuni ili kuepusha matumizi mabaya ya vyombo vya habari.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel amesema kuwa katika kufanya hivyo ni wajibu wa wadau wote kushirikiana
kutumia vyema maendeleo hayo ya tekinolojia kwa ajili ya ustawi wa jamii na
maendeleo ya taifa.
Profesa
Elisante alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa mashauriano
miongoni mwa wadau wa sekta ya habari kuhusu mapendekezo ya Kanuni za maudhui
yanayorushwa na vituo vya Utangazaji vya Redio na Televisheni na Kanuni za
Maudhui Mtandaoni.
“Ni
wajibu wetu kama taifa linalosimamia maadili na ambalo lingependa kudumisha
amani na mshikamano, kutunga kanuni ambazo zitahakikisha kuwa kunakuwa na
matumizi mazuri, sahihi na salama ya maudhui ya mtandaoni”Profesa Elisante
alisisitiza.
Aliwaambia
washiriki wa mkutano huo kuwa kuweka kanuni ni suala muhimu na kuwakumbusha matumizi
ya mfumo wa habari mtandaoni wakati mwingine umetumika kupotosha jamii, kujenga
chuki, kutoa habari za faragha za watu binafsi au habari zilizoleta sintofahamu
miongoni mwa jamii.
Aliongeza
kuwa kufanyika kwa mkutano huo ni jambo muhimu kwa kuwa washiriki watapata
fursa ya kujadili kanuni hizo ambazo baadhi zinadaiwa kuwa zimepitwa na wakati
na pia haziendani na utendaji na kazi katika ushindani wa soko.
Katika
mkutano huo ambao Profesa Elisante alikuwa mwenyekiti wake alieleza kuwa pamoja
na kuwa bado kumekuwepo na mijadala mikali katika nchi nyingi zikiwemo za Magharibi
kuhusu uwekaji kanuni lakini ukweli unabaki kuwa nchi hizo zimeweka sheria na
kanuni zinazosimamia matumizi ya intaneti.
“Ni
kweli kwamba tekinolojia hii ina changamoto katika usimamizi lakini hakuna
uhuru usio na mipaka. Kwa hiyo imekuwa ni wajibu wa kila nchi kutafakari
mahitaji na umuhimu wa kutoa miongozo itakayosaidia jamii na taifa” Alieleza
Profesa Elisante.
Mapema
akimkaribisha Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dk. Hassan Abassi aliwaeleza washiriki kuwa Mkutano huo ni muhimu katika
historia ya maendeleo ya tasnia ya habari nchini kuwa umelenga kuweka kanuni
bora zitakazoratibu tasnia.
“Tumeitana
hapa kushauriana kuhusu kanuni hizi hivyo hakuna haja ya kueneza wasiwasi kuwa
katika mitandao ya kijamii kuwa serikali imedhamiria kudhibiti vyombo vya
habari” Dk. Abbassi aliwaeleza washiriki.
Wakati huo huo, Serikali imeongeza muda wa siku saba
kwa wadau wa sekta ya utangazaji na mitandao kuwasilisha maoni yao kuboresha
kanuni zilizopendekezwa. Uamuzi huo umefikiwa mwishoni mwa mkutano wa
mashauriano kujadili kanuni hizo ambapo wadau wengi waliomba muda zaidi.
Akifunga
mkutano huo Profesa Elisante alisema ni vyema wadau wakaitumia fursa hiyo
kuwasilisha maoni yao kwa maandishi ili kuboresha kanuni hizo hatimae taifa
kuwa na kanuni bora kwa faida ya jamii yote.
Katika
maelezo yake kufunga mkutano huo Profesa Elisante aliwashukuru washiriki kwa
kutoa maoni yao na kuahidi kuwa serikali itayafanyia kazi maoni hayo.
Alieleza
kuwa ni ukweli kuwa vyombo vya habari vinafanya biashara na pia vina wajibu wa
kuelimisha jamii hivyo vitu viwili havina budi kwenda sambasamba bila kuathiri
upande mwingine.










0 Comments