Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akihutubia Jumuiya ya Shule ya
Sekondari Baobab, wakati wa mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa Kidato cha Nne
wanaotarajiwa kufanya mitihani yao siku chache zijazo.
Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Baobab Bw. Halfan Swai, akiiomba Serikali
iangalie changamoto ya riba ya mikopo inayotolewa an taasisi za fedha pamoja na
kuondoa kodi mbalimbali zinazotozwa shule binafsi kwakuwa taasisi hizo zinaisaidia
Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake, wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha
Nne ya Shule hiyo.
Meza
Kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb) (Katikati), wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha
Nne ya Shule mchanganyiko ya Sekondari Baobab, iliyoko eneo la Mapinga, Wilaya
ya Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo wanafunzi 149 wanatarajiwa kuhitimu masomo yao
majuma machache yajayo.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab, wakionyesha ishara ya umoja, upendo
na mshikamano wakati wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao wakati wa
Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya shule yao.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimkabidhi zawadi
mmoja wa wanafunzi mwenye ulemavu aliyefanya vizuri katika baadhi ya masomo
wakati wa sherehe ya kuwaaga, iliyofanyika shuleni hapo.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), (Katikati), akikabidhi
keki kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Baobab, iliyoko Mapinga, Bagamoyo,
mkoani Pwani, ikiwa ni alama ya kusherehekea siku yao ya kuagwa shuleni hapo.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari Baobab, Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa katika Picha ya
pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kuhitimu masomo
yao hivi karibuni, wakati wa sherehe ya kuwaaga shuleni hapo.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimpongeza binti
yake Samira anayetarajiwa kuhitimu masomo yake ya Kidato cha Nne katika Shule
ya Seondari Baobab, iliyoko Mapinga, Bagamoyo mkoani Pwani ambapo Naibu Waziri
alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Mahafali hayo ya Kidato cha Nne.
Familia
ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akiwa na
mumewe Dkt. Kachwamba, wakimpongeza binti yao Samira anayetarajiwa kuhitimu
masomo yake ya Kidato cha Nne katika Shule ya Seondari Baobab, iliyoko Mapinga,
Bagamoyo mkoani Pwani ambapo Naibu Waziri alikuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali
hayo ya 10 ya Kidato cha Nne.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
....
Benny Mwaipaja, WFM,
Pwani
SERIKALI imeahidi
kuyafanyiakazi malalamiko ya wamiliki wa shule za binafsi nchini kuhusu kodi
mbalimbali wanazotozwa kwa kuwa Serikali inathamini mchango mkubwa wa taasisi
binafsi za elimu katika mapambano dhidi ya adui ujinga.
Ahadi hiyo
imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa
sherehe za mahafali ya kumi ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Baobab,
iliyoko Mapinga, Wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.
Dokta Kijaji
amesema kuwa tayari Serikali imeondoa baadhi ya kodi kwa shule hizo ikiwemo
kodi ya mabango, Usalama mahali pa kazi-OSHA, Ada ya zimamoto, na kwamba kikosi
kazi kilichoundwa na Serikali kupitia upya kodi zingine zinazoonekana kuwa
kikwazo katika utoaji wa elimu, kinaendelea na kazi na matokeo yake yataonekana
hivi karibuni.
“Niko kwenye
kikosikazi kinachoshughulikia changamoto za kodi kwenye shule za watu binafsi
ninaamini suluhisho litapatikana kutokana na Serikali kuthamini mchango wenu
mkubwa katika kuwapatia vijana wetu elimu” alisema Dkt. Kijaji
Alieleza kuwa
katika Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2017/2018, suala hilo litazingatiwa na
kuwataka wamiliki wa shule binafsi nchini kuwa watulivu wakati jambo hilo
linafanyiwakazi tena kwa umakini mkubwa.
Awali Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari Baobab, Bw. Halfan Swai, pamoja na kuiomba
Serikali ifute kodi mbalimbali wanazotozwa kwa kuwa hawafanyibiashara bali
wanaisaidia Serikali kutoa huduma kwa jamii, ameomba pia isaidie kuangalia viwango vya riba vinavyotozwa na
taasisi za fedha nchini kwa kuwa zinawawekeka katika mazingira magumu
wanapohitaji mikopo ya kuendeleza shule zao.
Wanafunzi 149, (wavulana
14 na wasichana 135) wa Shule hiyo wanaotarajiwa
kuhitimu masomo yao ya kidato cha nne hivi karibuni, wameahidi kufanya vizuri
katika mitihani yao kwa kuwa wameandaliwa vizuri na walimu waliobobea katika
ufundishaji pamoja na mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunzia shuleni
hapo.
Dokta Ashatu
Kijaji, mbali na kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, yeye na familia yake
wameshuhudia mtoto wao Samira, akiagwa wakati wa mahafali hayo yaliyohudhuriwa
na watu mbalimbali wakiwemo wazazi, ndugu na jamaa wa wanafunzi hao.









0 Comments