Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA
Serikali
imewasilisha Mkataba wa Kimataifa wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta
ghafi la Afrika Mashariki kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Akiwasilisha
Mkataba huo kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison
Mwakyembe amesema kuwa Tanzania na Uganda ni wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambayo malengo yake ni pamoja na kuimarisha ushirikiano
kati ya nchi wanachama kwenye maeneo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii
kiteknolojia , utafiti, ulinzi na masuala ya Kisheria.
Dkt.
mwakyembe amesema kuwa Serikali ya Uganda kupitia kampuni za Kimataifa
za TOTAL, TULLOW NA CNOOC iligundua uwepo wa mafuta ghafi takribani
mapipa bilioni 6.5 katika eneo la Albertine nchini Uganda.
"
Kufuatia ugunduzi huo, Serikali ya Uganda ilianza kutafuta njia ya
kusafirisha mafuta hayo kwenda kwenye soko la kimataifa ambapo
iliaanisha njia takribani tatu ikiwemo ile ya kutoka Hoima nchini Uganda
hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania" amesema Dkt. mwakyembe.
Aidha
Dkt. mwakyembe amebainisha baadhi ya faida zitokanazo na Mkataba huo
ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya Serikali kutokana na Kodi ya zuio na
Kodi ya Mapato ya Kampuni zitakazotozwa wakati wa ujenzi na uendeshaji
wa Mradi.
Vilevile amesema kuwa Serikali ya
Tanzania itanufaika katika kuongezeka kwa mapato ya Serikali kwa
takribani Dola za Marekani 12.2 kwa kila pipa la mafuta ghafi
litakalosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga kulingana na kiwango cha
Hisa za Serikali ya Tanzania.
" kuimarika kwa
mahusiano ya kidiplomasia, ulinzi na usalama kati ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda pamoja na nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa ujumla sambamba na kuimarika kwa huduma mbalimbali katika
bandari ya Tanga kutokana na shughuli za Mradi na miundombinu
itakayojengwa" aliongeza Dkt. Mwakyembe
Pia
ongezo kwa fursa za ajira kwa Watanzania ambapo takribani watanzania
10, 000 wataajiriwa wakati wa ujenzi na ajira zipatazo 1,000 wakati wa
uendeshaji, Amesema Dkt. Mwakyembe.
Kwa upande
wake Deogratius Ngalawa akimuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Nishati na Madini ameishauri Serikali kuhakikisha inasimamia
utekelezaji wa mkataba huo kwa kuzingatia mustakabali wa manufaa ya
kiuchumi kwa Taifa.
" Napenda kutoa pongezi za
dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa juhudi zake na umahiri aliouonesha katika kuhakikisha
Tanzania inapata fursa ya mradi huu mkubwa wa ujenzi wa bomba la
kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania"
Amesema Ngalawa.
Akiongea kwa niaba ya Msemaji
Mkuu kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Devota
Minja amesema kuwa bomba hilo la kusafirisha mafuta ilikuwa na kazi
iliyohusu zaidi ushawishi mpana kwani kulikuwa na ushindani mkubwa utoka
kwa nchi jirani.

0 Comments