Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania ( TACAIDS), Jumanne Issango (kushoto) akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 21, 2017 wakati akitoa taarifa kuhusu majukumu ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI, mafanikio, changamoto na mwelekeo wa baadaye (kulia) Kaimu Mkurugenzi Idara ya mwitikio wa kitaifa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania ( TACAIDS), Audrey Njelekela .
Kaimu Mkurugenzi Idara ya mwitikio wa kitaifa Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania ( TACAIDS), Audrey Njelekela akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari.ambapo ameitaja mikoa inayoongoza kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa ni pamoja na Njombe na Iringa ambapo mikoa iliyo chini kwa maambukizi ni Manyara ,Tanga na Lindi.
Mkutano ukiendelea.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
(Picha zote na Philemon Solomon-Mtazamo News)
MAAMBUKI ya virusi vya ukimwi nchini yameteremka kutoka asilimia 5.7 kwaka 2007 hadi mwaka 2008 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011 na 2012.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugrnzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Jumanne Issango wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu majukumu ya tume hiyo, mafanikio, changamoto na muelekeo wa baadaye.
Alisema kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kinaendelea kupungua kutoka aslimia 0.32 kwa kipindi cha mwaka 2012 na kitafikia hadi 0.16 ifikapo mwaka 2018.
Issango alisema kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata huduma na tiba ya VVU ikiwa ni mapoja na dawa za kupunguza makali ya ukimwi kutoka watu 333,517 mwaka 2010 hadi kufikia 650,003 mwaka 2015 na kuanzisha na kuimarisha ofisi za waratibu wa ukimwi wa mikoa TACAIDS kwenye mikoa yote ya Tanzania Bara.
Aliongeza kuwa mpango mwingine ni kuwezesha mikoa 21 na Halmshauri 133 kuweka mifumo ya kuweza kutumia Tehama kwa utoaji taarifa na upashanaji wa habari na kuhifadhi data ya Tomsha.
Aliongeza kuwa kutakuwepo na kuanzisha mfuko wa udhamini wa shughuli za kudhibiti ukimwi (ATF) 2015 na serikali imeanza kuchangia sh.bilioni 3 kwa mwaka wa fedha wa 2015 na 2016.
Akizungumzia changamoto zilizopo Issango alisema ni upungufu wa rasilimali fedha za mapambano dhidi ya ukimwi kwa kuwepo kwa vyanzo vilivyo endelevu, unyanya paa katika jamii pamoja na uelewa mkubwa wa wananchi kuhusu ukimwi na kubadili tabia hakuendani na kiwango cha elimu ya ukimwi.
Alisema muelekeo na mataraji ni kutekeleza kwa ufanisi mfuko wa kudhibiti ukimwi ambapo serikali imeanzisha mfuko huo ndani ya tume ambapo utaweza kupanua wigo wa ukusanyaji rasilimali fedha ndani ya nchi na kuongeza ushiriki wa sekta isiyo ya serikali katika mapambano dhidi ya ukimwi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya mwitikio wa kitaifa, Audrey Njelekela, ameitaja mikoa inayoongoza kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuwa ni pamoja na Njombe na Iringa ambapo mikoa iliyo chini kwa maambukizi ni Manyara ,Tanga na Lindi.
Aidha ameeleza kuwa TACAIDS inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na unyanyapaa wanaokutana nao waathirika wa ugonjwa wa ukimwi, upungufu wa raslimali-fedha baada ya wafadhili kuondoka na kuongezeka kwa watoto yatima.
0 Comments