Nahodha wa timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi iliyoundwa na wachezaji kutoka kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto
na Uhamiaji Amina Juma Kizaba akipokea kombe la ushindi wa kwanza kutoka kwa
Mdadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali James A. Mwakibolwa
jana Tukuyu Mbeya baada ya kuilaza timu pinzani ya Kiimo Kijiji Kitulivu (KKR)
kwa mabao 26-16.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi iliyoundwa na wachezaji kutoka kutoka Jeshi la Polisi,
Magereza, Zimamoto na Uhamiaji wakifurahia ubingwa wao mara baada ya mechi jana
Tukuyu Mkoani Mbeya.
Wachezaji wa timu ya Ndato wakifanya mazoezi
kabla ya mechi yao dhidi ya timu ya Isange.
Wachezaji wa timu ya
Ndato (waliovaa jezi nyeupe) wakimenyanya na timu ya Isange (waliovaa jezi za
bluu) wakati wafainali ya Tamasha la Tulia Trust Tukuyu mkoani Mbeya.
Picha na Eleuteri
Mangi,WHUSM, Tukuyu)
.....
Na Eleuteri Mangi,
WHUSM, Tukuyu.
Washindi wa mchezo wa
soka na mpira wa pete wapokea kitita cha wamepokea kitika cha Sh. 7,500,000/=
katika Tamasha la Ngoma za Jadi linaloratibiwa na Taasisi ya Tulia Trut wilayani
Tukuyu mkoa wa Mbeya.
Tamasha hilo
limeifanya wilaya ya Tukuyu kuendelea kung’ara katika tasnia ya michezo kwa
kupambwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka, mpira wa pete na ngoma za jadi
ambapo tamasha hilo linatarajiwa kuhitimishwa Septemba 23 mwaka huu na
kuongozwa na kaulimbiu “Tuuenzi Utamaduni wetu”.
Uwanja wa Tulia ambao
awali ulikuwa unaitwa Tandale ulifurika mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya
mkoa huo na mikoa inayoshiriki tamasha hilo wameshuhudia timu za Ndato na
Isange zilipokutana kumenyana katika hatua ya fainali ambapo Ndato ndio
walioibuka kidedea kwa kuwalaza Isange kwa mabao 2-1.
Mchezo huo ulianza
kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao la mapema ambapo dakika ya pili kipindi
cha kwanza Ndato ndio waliofanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na
mchezaji Monte Stephano.
Mashambulizi ya
kushtukiza yaliendelea kwa kila upande ili kutafuta ushindi, dakika ya 18
kipindi cha kwanza Isange walipata bao la kusawazisha kupitia kapteni wake Hussein
Mwalugaja, bao lililozipeleka timu zote kwenye mapumziko kwa kufungana goli 1-1.
Kipindi cha pili
kilianza kwa vuta nikuvute ambapo Ndato ndio walifanikiwa kupata bao la
kuongoza ambapo hadi kipenga cha mwisho Ndato ndio walioibuka kidedea kwa mabao
2-1.
Kwa upande wa mpira
wa pete, timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyoundwa na wachezaji
kutoka kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji waliwalaza timu
pinzani ya Kiimo Kijiji Kitulivu (KKR) kwa mabao 26-16.
Kwa ushindi huo,
bingwa ambao ni timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepata zawadi ya
kombe, medali na kujipatia kitita cha Sh. 1,500,000/= wakati mshindi wa pili
ambaye ni timu ya KKR nayo ikijipatia kombe, medali na kitita cha Sh.
1000,000/= huku mshindi wa tatu
akijipatia sh. 750,000/= na mshindi wa nne akiweka kibindoni sh.500,000/=
Akizungumzia tamasha
hilo linaloendelea hadi Sptemba 23 mwaka huu, Mwasisi wa Taasisi ya Tulia Trust
ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Tulia Ackson amesema kuwa wamejipanga kulifanya tamasha hilo kuwa endelevu na
kuwa na wigo mpana zaidi na hatimaye kufikia nchi nzima.
Dkt. Tulia Ackson
amewashukuru wadhamini kwa kufanikisha tamasha hilo na kuwa waomba waendelee
kujitoa kwa lengo la kuijenga Tanzania yenye utamaduni imara unaotoa ajira na
kulinda maadili ya Kitanzania.
Wadhamini hao ni
pamoja na Benki ya CRDB, Ubalozi wa China, Umoja wa Mataifa (UN), Ubalozi wa Ujerumani, Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), Bodi ya Utalii Tanzania, PPF, WCF, Vodacom, TCRA,
pamoja na Kampuni ya TOL Gas Ltd.




0 Comments