Baadhi ya wawakilishi
wa Bodi ya Kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC), wa kwanza
kutoka kulia ni Mwenyekiti wa UNECA, Dkt. Koja Busia, Mwenyekiti wa Bodi,
Masresha Gebreselassie, Mwenyekiti wa AUC, Frank Mugyenyi na Mkurugenzi Mkuu wa
AMGC, Ibrahim Shaddad.
Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (anayeongea). Wengine ni
washiriki katika kikao hicho.
Mshauri Mwelekezi wa
AMGC, Timo Gawronski akitoa maelezo kwa washiriki wa kikao wakiwa katika maabara ya uchunguzi wa asili ya madini husika.
Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati) baada ya kufugua
kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Nchi Wanachama wakiwa katika Kituo cha Afrika
Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC). Wengine ni Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin
Mchwampaka (kushoto) na Assa Mwakilembe (kulia).
Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati mstari wa mbele)
akiwa katika picha ya pamoja ya Mkutano wa MakatibU Wakuu kutoka Nchi Wanachama
wa Kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (AMGC). Wengine katika
picha ni wawakilishi kutoka Nchi wanachama pamoja Makamishna na Wakuu wa Vituo
vya Madini.
Tanzania imekuwa Mwenyeji wa Mkutano wa 37 wa Masuala ya
Kisera ya Kituo cha Afrika cha Sayansi ya Jiolojia na Madini (African Minerals and Geosciences Center
(AMGC) ambao unafanyika jijin Dar es Salaam.
Awali, mkutano huo ulianza kwa kuwakutanisha Wakurugenzi wa
Bodi ya kituo hicho na kufuatiwa na mkutano wa tarehe 13 Agosti, 2017, uliowashirikisha
Makatibu Wakuu kutoka nchi Wanachama wa kituo husika.
Akizungumza na Vyombo vya Habari wakati wa Mkutano wa
Makatibu Wakuu, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James
Mdoe alisema lengo la kukutana ni kufanya tathmini na kuendeleza yale
yaliyopangwa kutekelezwa na nchi wanachama ikiwemo kupanga mipango ya mwaka
ujao na bajeti ya utekelezaji wa mipango
hiyo.
Profesa Mdoe alisema kuwa yapo mambo ambayo waliyokubaliana
katika mkutano wa 36 yakiwemo ujenzi ya Maabara ya kisasa kwa ajili ya nchi za
Maziwa Makuu ambayo itasaidia katika shughuli za madini ikiwemo za uchunguzi wa
madini, kukiwezesha kituo hicho kufanya shughuli zake vizuri na kusaidia nchi
wanachama katika sekta husika.
Akizungumzia manufaa ya kituo hicho nchini, alisema kuwa
kituo hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania hususan Taasisi za Vyuo
Vikuu nchini ambazo zimekuwa zikikitumia Kituo hicho katika mafunzo mbalimbali.
“Sisi tumepata bahati kubwa ya kuwepo kwa kituo hiki hapa
nchini. Tayari vipo Vyuo na wanafunzi ambao wamenufaika na uwepo wa kituo hiki.
Kwetu sisi ni faida kwa sababu hatutumii gharama kubwa za kufuata huduma
zinazotolewa na kituo hiki tofauti na nchi nyingine ambazo zipo mbali,” alisema
Prof. Mdoe.
Aidha, alisema faida nyingine kwa nchi wanachama waliolipa
ada kamili ni kupata punguzo la asilimia 40 la kutumia maabara za Kituo hicho.
Akizungumzia malengo ya baadaye ya kituo hicho, alieleza kuwa
ni kukifanya kuwa kituo bora zaidi ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama kutoka
nchi nane zilizopo sasa.
Hadi sasa nchi wanachama ni Tanzania, Msumbiji, Sudani
Kaskazini, Ethiopia, Uganda, Kenya, Comoro na Angola.
Sambamba na mkutano huo, itafanyika pia sherehe ya
kuadhimisha miaka 40 ya kituo husika tangu kuanzishwa kwake.
0 Comments