Random Posts

Wahandisi wasisitiza Wasichana kujituma masomo ya sayansi lindi.

 Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Bi. Liberatha Alphonce, akielekeza jambo kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Nachingwea mkoani Lindi, kuhusu umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hesabu. 
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Nachingwea mkoani Lindi, wakimsikiliza Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, Bi. Liberatha Alphonce (hayupo pichani), alipofika shuleni hapo kuhamasisha umuhimu wa masomo ya Sayansi na Hesabu.
 Maabara ya Shule ya Sekondari ya wasichana ya Nachingwea mkoani Lindi, licha ya kukamilika lakini bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa.
 Jengo la maabara la Shule ya Kutwa ya Nachingwea Sekondari, ambalo halijakamilika kutokana na uhaba wa fedha, hali inayopelekea wanafunzi hushindwa kujifunza masomo ya sayansi kwa vitendo kutokana na changamoto hiyo.
Wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara, wakisikiliza maoni kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kilwa, mkoani Lindi (hawapo pichani), walipofika shuleni hapo kuhamasisha usomaji wa masomo ya Sayansi na Hesabu kwa wasichana.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Post a Comment

0 Comments