Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya
barabara, Bi. Liberatha Alphonce, akionesha mfano wa picha iliyochorwa kwa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchinga mkoani Lindi (hawapo pichani), ili
kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchinga mkoani Lindi,
wakimsikiliza Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya
barabara, Bi. Liberatha Alphonce (hayupo pichani) wakati akitoa mada kuhusu
uhamasishaji wa masomo ya Sayansi kwa wasichana.
Wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala
ya barabara, wakisikiliza maoni kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Mchinga mkoani Lindi walipotembelea shule hiyo kuhamasisha usomaji wa masomo ya
Sayansi kwa wasichana.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mchinga mkoani Lindi,
wakionesha ndoto zao kwa Wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika
masuala ya barabara, walipotembelea shule hiyo kuhamasisha usomaji wa masomo ya
Sayansi kwa wasichana.
Mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Lindi, akitoa maoni yake
kuhusu changamoto zinazokabili shule yao kwa Wahandisi wa kike
kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Kitengo
maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya barabara.
Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Ujenzi), Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya
barabara, Bi. Rahma Mwinyi, akigawa zawadi ya madaftri kwa wanafunzi wa shule
ya Mkonge mkoani Lindi ili kuhamasisha wanafunzi hao kupenda masomo
ya sayansi.
Walimu
wa masomo ya Sayansi mkoani Lindi wameiomba Serikali kuchukua hatua za
haraka za kuandaa na kuimarisha miundombinu bora kwa shule za Sekondari
zinazofundisha masomo hayo ili kuendeleza na kufufua vipaji vya wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba ya walimu hao wakati wa ziara iliyofanywa na wahandisi wa
kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
kupitia Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya
barabara katika shule za mkoa huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Mchinga iliyopo mkoani humo, Bw. Makopa Selemani ,
amesisitiza kwa Serikali kuona namna ya kujenga maabara nyingi za sayansi
ambazo zitakuwa na vifaa na kuongeza walimu wa Sayansi ambao wameonekana kuwa
ni wachache katika mkoa huo.
"Tunaiomba
Serikali kutazama kwa jicho la pekee shule za mkoa huu hususan zenye michepuo
ya sayansi kwani si kwamba wanafunzi hawapendi masomo haya bali miundombinu
hairidhishi", amesema Mwalimu Mkuu.
Aidha, Mwalimu
Mkuu ameongeza kuwa ili kuwasaidia wanafunzi wa kike katika mkoa huo serikali
iwajengee mabweni wanafunzi hao ili kuepusha kupata vishawishi kwani wengi
wao wanaishi mbali na shule.
Mwalimu
Mkuu Selemani, ameelezea baadhi ya mikakati ya shule yake katika kuhamasisha
wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi ikiwemo kufanya vikao vya mara kwa
mara na wanafunzi hao ili kujadili changamoto zao na kuzitatua.
Ametoa
wito kwa Wizara kufanya ziara za mara kwa mara katika shule mbalimbali nchini
ili kuhamasisha wanafunzi husasan wa kike kupenda na kujifunza masomo ya
sayansi ambayo yameonekana kuwa ni vikwazo katika mkoa huo.
Kwa
upande wake, Mhandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Ujenzi), kupitia Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika
masuala ya barabara, Bi Liberatha Alphonce, amewasisitiza
wanafunzi wa kike mkoani humo kuanza kujituma na kujijengea misingi imara
ya kupenda masomo ya sayansi wakiwa katika ngazi za awali ili kufikia malengo
yao.
Amefafanua
kuwa masomo ya Sayansi yanatoa fursa za kujiajiri na urahisi wa kupata mikopo
kwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na elimu ya juu.
Naye,
mwanafunzi Shamira Salum, kutoka shule ya Sekondari ya Mchinga, ameiomba
serikali kuongeza walimu na vifaa katika shule za mkoa huo ili kuweza kutimiza
malengo yao ya kuwa wahandisi na madaktari wa baadae.
Ziara
ya wahandisi wa kike kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Ujenzi), kupitia Kitengo maalum cha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala
ya barabara imelenga kutoa elimu na kuhamasisha wanafunzi wa kike nchini kusoma
masomo ya sayansi ambapo pamoja na mambo mengine wahandisi hao wametembelea
shule ya sekondari ya Mchinga, Lindi, Mkonge na Mingoyo ambazo zipo mkoani
Lindi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano







0 Comments