Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango (katikati) akiwa na viongozi wengine wa
Serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga (kushoto), Kamishna Mkuu
wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA Charles
Kichere(kulia) wakiangalia Mzigo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akisoma maelezo ya mzigo huo ambayo
yalikuwa tofauti kabisa na uhalisia mara baada ya kuhakikiwa na timu ya Wataalamu wa Kitanzania wazalendo.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akiangalia Mzigo huo wa Almasi kutoka
kwenye kampuni moja ya uchimbaji wa madini hayo Mwadui mkoani Shinyanga, mara
baada ya kuhakikiwa na Wataalamu Wazalendo waligundua kuwa mzigo huo una uzito Kg. 29 tofauti na
Kg.13 zilizoanishwa na wahusika wa mzigo huo, na thamini yake ni zaidi ya Tsh.
Bilioni 64.
Sehemu
ya Mzigo huuo wa Almasi uliokamatwa katika uwanja wa Ndege ambao thamani yake
ni zaidi ya Tsh. Bilioni 64.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Filip Mpango akizungumza wakati akipokea Ripoti ya
Uchunguzi wa Madini hayo ya Almasi jijini Dar es Salaam.
Profesa
Abdulkarim Mruma akiwasilisha Taarifa yake ya Uchunguzi wa Madini yaliyokamatwa
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Picha na Mpiga Picha Maalum













0 Comments