Rais wa WCB, Diamond Platnumz bado yupo kwenye kitimoto baada ya kuthibitisha kupata mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobetto.
Hatua hiyo imechukua sura mpya baada ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe.
Awali katika maelezo yake mwanamuziki Diamond amesema ameshazungumza
na mpenzi wake huyo kuhusiana na mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba
ameelewa na hakuna tatizo tena.
Wakati Diamond akiendelea na mahojiano katika kituo cha Clouds FM,
Zari aliandika katika mtandao huo akisema: “Hahahaha unajidanganya,
unasema uongo kuhusu mimi kujua kuhusu michepuko yako, malizana na balaa
ulilolianzisha. Mimi kunyamaza haimaanishi ni mpumbavu. Kuwa makini na
maneno yako.”
Aliendelea kuandika: “Inawezekana mimi ni mama wa watoto wako ndio
maana nimeamua kunyamaza kimya. Labda ugoogle kuhusu ‘defamation of
character law suit’, usinijaribu.”
Diamond alipoulizwa kuhusu kauli hizo amesema anamwelewa kwa kuwa
kuna baadhi ya mambo hakumweleza na kwa mara ya kwanza huenda ameyasikia
wakati huo


0 Comments