Mkurugenzi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi
akimkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho mwakilishi wa Jarida la PLUS 255
MAGAZINE Bw. Francis Maduhu mara baada ya kukamilisha taratibu za usajili leo
Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni kwa machapisho linafuatia
utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick Kipangula.
Mwakilishi wa
Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu akionyesha Leseni ya machapisho
aliyokabidhiwa kwa ajili ya Jarida lake leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la
utoaji wa Leseni za machapisho linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha
Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016.
Mkurugenzi wa
Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza
mwakilishi wa Jarida la PLUS 255 MAGAZINE Bw. Francis Maduhu baada ya
kumkabidhi Leseni ya Usajili wa machapisho kufuatia kukamilisha taratibu za
usajili leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi la utoaji wa Leseni za machapisho
linafuatia utekelezaji wa kifungu namba 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari ya
mwaka 2016. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Usajili Bw. Patrick
Kipangula.
Picha na: Idara ya
Habari - MAELEZO



0 Comments