Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na baadhi ya wadau wa afya kutoka Shirika
linaloshughulikia maswala ya ukimwi kutoka Umoja Wa Mataifa(UN Aids) na Wizara ya Afya , kushoto kwake ni
Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi
Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe
Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango
Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael
Sidibe wa kwanza kulia akiongea na baadhi ya watendaji wa sekta ya Afya hawapo
pichani wakati alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara hiyo leo jijini Dar es
salaam , kushoto ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi wa Ubora wa Hudum za Afya nchini Dkt. Mohammed Mohammed kushoto
akifuatilia mazungumzo kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa maongezi na Mkurugenzi Mtendaji wa UN Aids
Bw. Michael Sidibe hayupo pichani , kulia ni Mkurugenzi wa Kinga Wizara
ya Afya Dkt. Neema Rusibamayila .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kulia akiongea na Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La
Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe wa pili kushoto mara baada ya
kuwasili kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo jijini Dar es salaam , wa kwanza kulia ni
Mkurugenzi wa ESA Bi. Catherine Sozi na
wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi
mwakilishi nchini Leo Zekeng .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe wa pili kulia , wengine
ni Mkurugenzi mwakilishi nchini Leo Zekeng wa kwanza kushoto na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa
Kanda ya ESA Bi. Catherine Sozi mara
baada ya maongezi wakati
alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara hiyo
leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akishikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji Wa
Shirika La Umoja Wa Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe mara baada ya maongezi wakati alipotembelea Ofisi ndogo za Wizara hiyo leo jijini Dar es
salaam.
...
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
Asilimia 95 ya kina mama wajawazito hufikiwa na huduma ya
kupima maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU) ili kuweza kujifungua salama
watoto ambao hawana hatari ya kupata maambukizi hayo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa Mataifa
La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw.
Michael Sidibe wakati alipotembelea ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es
salaam leo.
?Hata hivyo asilimia 90 ya walio na maambukizi wamepata dawa
za ARV hii imepelekea maambukizi ya VVU
toka kwa mama kwenda kwa mtoto kupungua katika asilimia 21 mwaka 2009 hadi 7.6
mwaka 2015? alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisisitiza kuwa tunaweka nguvu zaidi kwa
vijana na hasa wa kike na vijana walio katika makundi maalum yenye hatari zaidi
ya kuambukiza au kuambukizwa VVU.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania imepiga
hatua katika mapambano zidi ya UKIMWI ili kufikia malengo ya
kutokomeza janga hilo la kiafya katika
jamii ifikapo mwaka 2030 kwani maambukizi yamepungua toka asilimia 7.1 mwaka
2007/8 hadi kufikia asilimia 5.1 mwaka 2011/12.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Umoja Wa
Mataifa La Mpango Wa Ukimwi Duniani (Unaids) Bw. Michael Sidibe amesema kuwa wafadhili wanachangia sehemu kubwa ya muitikio
wa mapambano ya UKIMWI hivyo UNAIDS wako tayari kusaidia katika kuandaa mpango
endelevu ili kuhakikisha Fedha za
wafadhili zikipungua huduma ziendelee.
Aidha Bw. Sidibe amesema kuwa Shirika la UNAIDS limeanzisha
mpango wa kuwezesha nchi za Afrika kuwa na wahudumu wa afya ngazi ya Jamii ambao
watasaidia kuboresha mfumo mzima wa Sekta ya Afya.
Mbali na hayo Bw.
Sidibe ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa hatua kubwa
iliyofikiwa katika mapambano ya UKIMWI nchini, hususani kuweza kufikia
takribani Waathirika 935,228 wanaotumia dawa za ARV ifikapo Juni 2017.






0 Comments