Mkurugenzi
wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Sanjay Rughani (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya
mabenki, Bi Heidi Toribo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la 'Women's World Banking', Tom Jones akizungumza.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo.
.....
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania,
Sanjay Rughani alisema kongamano hilo litakalowakusanya pamoja wanawake
viongozi katika fani mbalimbali zikiwemo
za Mabenki, Teknolojia, Wafanyabiashara na Mashirika ya Umma na Mashirika
binafsi litakuwa la siku mbili.
Rughani
aliyeambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la 'Women's World, Banking na
Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, alisema kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele
kuwawezesha wanawake kupata mitaji ya kifedha na kuwaelimisha wanawake kuhusu
masuala ya fedha na uchumi.
Aidha
aliongeza kuwa, mambo mengine wanayowawezesha wanawake ni kutoa bidhaa maalum
za kibenki ikiwa ni pamoja na
kuwawezesha kupitia miradi yake ya kijamii.
"Wanawake
wana mchango mkubwa katika maendeleo ya chumi za nchi na tumejizatiti
kikamilifu kuwawezesha wanawake kuwa uhuru wa uchumi na fedha, kupata mitaji na
kuwa na elimu ya mambo ya fedha na uchumi. Kama benki tutaendelea kumuwezesha
mwanamke wa Kitanzania kuwa gurudumu la maendeleo la nchi yetu," alisema
Rughani.
Rughani
aliongeza kuwa, kongamano hilo litawahusisha wanawake 300 kutoka nchi
mbalimbali duniani ambao wataongelea maudhui yanayohusu kujumuishwa kwa wanawake katika
mambo ya kifedha.
Washiriki
watajumuisha viongozi wanawake wa sekta mbalimbali kama tekenolojia,
uwekezaji,, viwanda, mabenki na mashirika ya kifedha pamoja na wanachama wa
shirika la 'Women's Word Banking kutoka nchi 32.
"Benki
ya Standar Chartered inaamini kuwa kongomano hili litaleta mageuzi ya kiuchumi
na kuwawezesha wanawake kuwa wadau wakuu katika kuleta maendeleo nchini
Tanzania na katika nchi mbalimbali ambazo zitashiriki," alisema Rughani.
Naye Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la 'Women's World Banking', Tom Jones alisema washiriki
mbalimbali kutoka sekta tofauti ni ushuhuda mkubwa kwamba wa jinsi ambavyo
wanazidi kuchacharika katika kuleta maendeleo ya kiuchumi ya nchi zao.
Kwa upande
wake, Bi Heidi Toribo ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kitengo cha Biashara kati ya
mabenki akizungumza na wanahabari waliohudhuria hafla hiyo alisema;
"Mwanamke
anayejiweza kiuchumi anasaidia siyo tu biashara yake bali pia na familia yake
kwani anakuwa ni mtaji mkubwa kwa jamii yake na kwa maendeleo ya nchi kwa
ujumla."
Kongamano
hilo litafanyika wakati Benki ya Standard Chartered Tanzania ikiwa inaadhimisha
miaka mia moja tangu ifungue biashara yake nchini Tanzania.
Katika kuadhimisha
mafanikio yake iliwakaribisha nchini zaidi ya viongozi 40 kutoka Mabara ya
Afrika na Asia mwezi Machi mwaka huu. Viongozi hao walikutana na viongozi
mbalimbali wa kiserikali, wateja, wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni njia
mojawapo ya kuthibitisha dhamira yake ya kuendelea kufanya biashara nchini kwa
lengo la kusaidia kukuza uchumi wa nchi.
Makamu wa
Rais Mama Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi
wa kongamano hilo.
0 Comments