Mwenyekiti mteule wa Chama Cha Wafanyakazi mkoa wa Dar es salaam, Mziwanda Chimwege (kushoto) akionesha
chati cha ushindi kwa wajumbe mara baada ya kukabidhiwa na msimamizi wa
uchaguzi Emmy Rweyendela kulia baada ya kuwabwaga wenzake wanne, uchaguzi uliofanyika Oktoba 20, 2017 Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA KHMISI MNUSSA)
Msimamizi wa
uchaguzi Emmy Rweyendela (kulia) akitangaza matokeo mara baada ya kupatikana mshindi
Katibu (TUGHE) mkoa, Gaudensi
Kadyango alianza kwa kuwashukuru wajumbe kwa kazi nzuri ambayo wameifanya na pamoja na madongo lakini napenda kuwahakikishia ni moja ya kipimo cha uongozi na ninjia ya kutaka kufikia malengo , alisema Kadyango.
Pamoja na kutaka kumtoa Katibu anaye ongea lakini najua ni changamoto za kazi lakini nitaendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano mkubwa na pia naomba haya yaliyoongelewa hapa yaishie hapahapa na mimi nipo na moyo mweupe na ninajua ni mambo ya kazi, aliendelea kusema.
Napenda niwahakikishie kwamba mimi ni mkomavu na niwatowe hofu nipo pamoja na ninyi kwa moyo mweupe na msisite kwa lolote na ninajuwa nichangamoto ya kupenya katika kufika mtu anapopataka kufika.
Napenda kuchukua fulsa hii ya kumpongeza Mwenyekiti mteule na kukuhakikishia sisi makatibu wa mikoa na wajumbe hawa tunakupa ushirikiano wa kutosha ili ufikie malengo yako na tuanzie kwenye matawi na kama sisi wenyewe kama viongozi.
Ndugu wajumbe na omba tuwe mfano kwa kuanzia katika matawi na utaongoza mikoa mitatu nayote utahakikisha unatimiza wajibu katika mikoa hiyo alisema Kadyngo
Mwenyekiti Kamati ya Wanawake (TUGHE) Taifa, Dokt. Jane Madete (kushoto) aliomba kumpa ushirikiano Mwenyekiti huyo kutoka katika Kamati tendaji matawi, mikoa na hata ngazi ya Taifa kwa yale yatakayohusu mikoa na tunakupongeza sana
Mwenyekiti mteule mkoa wa Dar es salaam, Mziwanda Chimwege akizungumza jambo mara baada ya kuchaguliwa kukiongoza Chama hicho kwa miaka mitano
Msimamizi wa
uchaguzi, Emmy Rweyendela (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi Mwenyekiti mteule mkoa wa Dar es salaam, Mziwanda Chimwege katikati na kushoto ni Katibu (TUGHE) Mkoa, Gaudensi Kadyango
Mwenyekiti mteule Mziwanda Chimwege (wa pili kulia waliokaa) katika picha ya pamoja na wajumbe
Baadhi ya wagombea waliokosa kinyanganyiro hicho , Almas Mzee
amempongeza Mwenyekiti huyo mpya na kuahidi kumpatia ushirikiano ili
kuleta tija.
Mwenyekiti mteule akizungumza na waandishi wa habari (pichani hawapo) alisema
Namshuru Mungu kwa nafasi hii kutokana na usimamizi bora wa sera nilizo jipangia ambazo zitakazomlinda mfanyakazi, pamoja na kufufua matawi ngazi za mkoa ili kutetea masilahi ya wafanyakazi na watumishi ndani ya chama. Ameongeza kuwa uwazi wa matumizi na mapato ya fedha utakuwa wa usawa ili kumlinda mtumishi katika kazi kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa sera yake ya HAPA KAZI
0 Comments