Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa
Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu
kushoto), wakati alipokagua daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Meneja wa Wakala wa
Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina (wa tatu kushoto),
akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (aliyevaa fulana nyeusi), wakati alipokagua daraja la Kinambo lililopo
katika barabara ya Kasansa-Muze KM
31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani
Rukwa.
Mafundi wakiendelea na
kazi ya ujenzi wa daraja la Kinambo lililopo katika barabara ya Kasansa-Muze KM 31.90 wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa.
Muonekano wa mitambo
ya kuchimbia nguzo za Daraja la Mto Momba unaounganisha mikoa ya Rukwa na
Songwe.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi
wa Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering (Groups) Corporation, wakati akikagua
maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa na
Songwe.
Mbunge wa Jimbo la
Kwela Mhe. Ignas Malocha, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati wa mkutano na wananchi wa
Kilymatundu mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Momba, wilayani
Sumbawanga.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wananchi wa
Kilymatundu mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mto Momba,
wilayani Sumbawanga.
Mmoja wa wananchi wa
kijiji cha Kilyamatundu kilichopo wilayani Sumbawanga akimkabidhi Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ushahidi wa picha za
miti iliyokatwa katika shamba lake kupisha mradi wa ujenzi wa Daraja la Mto
Momba, mkoani Rukwa.
Imeelezwa kuwa
kukamilika kwa Daraja la Mto Momba linalounganisha mikoa ya Rukwa na Songwe
kutafufua fursa za kiuchumi katika mikoa ya magharibi na kuongeza kasi ya
uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo alipokagua
ujenzi wa daraja hilo na kuwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Sumbawanga kuwa
Serikali imejipanga kuhakikisha daraja hilo linakamilika mwezi Agosti mwakani.
“Toeni ushirikiano
unaostahili kwa mkandarasi ili Daraja hili la Momba na madaraja madogo saba
yanayojengwa katika barabara ya Kasansa-Kilyamatundu yenye urefu wa KM 210.38
yakamilike kwa wakati”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa
amesisitiza nia ya Serikali ya kujenga barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM
210.38 na Stalike-Kilyamatundu-Mloo KM 500 kwa kiwango cha lami ili kuongeza
kasi ya uzalishaji na usambazaji wa mazao ya kilimo na mifugo katika Bonde la
Mto Rukwa kwenda maeneo mingine ya nchi.
“Wale wote ambao
wamewekewa alama za kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara nawaomba
wafanye hivyo mapema ili kuwawezesha wakandarasi kufanya kazi zao kwa uhuru na
kuiwezesha TANROADS kufanya usanifu wa kina”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye Meneja wa Wakala
wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina, amemhakikishia
Prof. Mbarawa kuwa watamsimamia kikamilifu mkandarasi anayejenga Daraja la Momba
na madaraja madogo saba katika barabara ya Kasansa-Kilyamatundu KM 210.38 ili
kazi ujenzi huo ukamilike kwa wakati.
Kwa upande wake Mbunge
wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha, amewataka wananchi watakaopata fursa za
ujenzi wa madaraja hayo kuepuka vitendo vya wizi na hujuma kwa wakandarasi.
Amesema kukamilika kwa
Daraja la Momba kuna manufaa mengi kiuchumi, kijamii kwa kuwa daraja hilo
litawaunganisha wakazi wa jimbo lake na mkoa wa Songwe na hivyo kuharakisha
shughuli za kimaendeleo.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano
0 Comments