Maudhui
ya Mkutano huo ni Kuimarisha Demokrasia kwa ajili ya kuwezesha Mtangamano Endelevu.
Mada
katika mkutano huo ni pamoja na : Kuheshimu Haki za Binaadamu na Nguvu ya Umma;
Chagamoto na utekelezaji wake. Burundi inawasilisha mada hiyo.
Aidha
Kenya itawasilisha mada ya Kuimarisha Uwajibikaji katika Utawala wa Sheria.
Rwanda
itawasilisha mada ya Uadilifu wa Maadili katika Kampeni za Kisiasa na Tanzania
itawasilisha mada ya Kuimarisha Mtangamano kupitia Uwazi katika Usimamizi wa
Mikataba ya Ununuzi wa Umma.
Mkutano
huo wa siku mbili umeanza leo Jumanne na utamalizika kesho Jumatano.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba akifungua Mkutano wa 6
wa Mwaka wa Utawala Bora Afrika
Mashariki unaofanyika jijini Arusha Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mbele katika picha Mhe. Said Hassan Said,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye ni Mkuu wa Ujumbe
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Mkutano huo.
Baadhi
ya Wajumbe wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliohudhuria
Mutano wa 6 wa Utawala Bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa
Mkutano huo leo jijini Arusha.
Wizara ya Mambo ya Nje na
ushirikian wa Afrika Mashariki
Othman M. Othman



0 Comments