NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile.
NA WAMJW-MWANZA
NAIBU Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa wadau wa sekta ya afya na watoa
huduma za afya hasa wauguzi na wakunga wanatakiwa kujikita zaidi kwenye kuokoa
na kuboresha afya ya mama mjamzito na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na
uzazi.
Akizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Ukunga
salama (More and Better Midwives) uliofanyika leo katika Chuo cha Uuguzi na
Ukunga Bukumbi kilichopo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza.
Sisi sote tunafahamu umuhimu wa wauguzi na wakunga katika
kuimarisha afya ya mama na mtoto hivyo Serikali ya awamu ya tano tumejipanga
kuhakikisha kuwa tunapunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya mama na mtoto? alisema
Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile alisema kuwa Serikali inafahamu kuna
changamoto ya upungufu wa watumishi katika kada mbalimbali za afya pamoja na
nyinginezo na wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwa kutoa kipaumbele cha ajira za
wauguzi na wakunga.
Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewaonya wakunga na wauguzi
wenye tabia ya kutumia lugha chafu kwa
wagonjwa pamoja na kuacha vitendo vya kuwaomba rushwa kwani fani hiyo
inaendeshwa kwa taaluma na maadili.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Misungwi Bw. Juma Sweda
amesema kuwa wananchi wa Wilaya hiyo wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika
kukata bima za afya kwani husaidia kuokoa gharama nyingi pindi wanapopata
maradhi na mpaka hivi sasa wananchi wenye bima ta afya inakadiriwa ni 9100.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Ukunga Salama nchini Dkt. Julius
Masanika amesema kuwa mradi huo utafadhili wanafunzi wa kanda ya ziwa na kanda
ya magharibi wanaojiunga na vyuo vya Uuguzi na Ukunga wasio na uwezo kwa
kuwalipia ada pamoja na mahitaji mengine.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Uuguzi na Ukunga katika Chuo cha Bukumbi ambaye anafadhiliwa
na mradi huo Rose Julius amesema kuwa anawasihi wanafunzi wafanye bidii kwenye
masomo ya sayansi na hatimae wachukue fani ya uuguzi na ukunga katika
kukabiliana na changamoto za vifo vitokanavyo na uzazi.
Mbali na ufunguzi huo wa mradi wa Ukunga salama unaojulikana
kama ?More and Better Midwives? ambao
umeshirikisha taasisi isiyo ya
Kiserikali JHPIEGO ,wawakilishi kutoka Chama cha wakungwa Canada(CMA) na Chama cha wakungwa Tanzania TAMA pia alitembelea Zahanati ya
Kambi ya wazee Bukumbi,Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Mwanza Sekou Toure ili kujua hali ya upatikanaji wa dawa .

0 Comments