Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akikabidhiwa ua na Afisa Utumishi
Bi. Daina Lumelezi wakati alipotembelea Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akiwasili Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akizungumza na watumishi wa Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akizungumza na watumishi wa Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bw.
Marcel Katembo akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Watoto.
Sehemu ya Watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akibadilishana mawazo na viongozi
wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii mara baada ya kumaliza kuzungumza na
watumishi wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi pamoja na watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati
alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO WAMJWW
Na
WAMJWW
Naibu Waziri wa Afya Maendelo
ya Jamii jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile ameitaka Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii kuratibu shughuli znazofanywa na
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili yafanye
kazi kulingana na uanzishwaji wa mashirika hayo.
Dokta Ndugulile aliyasema hayo
jijini Dar es Salaam wakati akizungumza
na watumishi wa Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii alipokwenda kujitambulisha kufuatia kuteuliwa hivi karibunoi katika mabadiliko yaliyofanyika ya baraza la mawaziri.
Alisema , pamoja na idara hiyo
kuwa na kanzi data kwa ajili ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini lakini
kuna haja ya kufuatilia utendaji kazi wa
mashirika yasiyo ya kiserikali kwani baadhi
ya mashirika hayo yamekuwa yakienda kinyume na kazi iliyokusudiwa.
‘”kuna mashirika yasiyo ya
kiserikali ya Kimataiafa na yale ya kitaifa ni vizuri yale ya kimataifa yawe na
sura ya kimataifa nay ale yenye sura za kitaifa yabaki na sura hiyo kwani wakati mwingine hasa kipindi cha
uchaguzi baadhi ya mashirika hayo hujishughulisha
na shughuli za kisiasa na kuacha malengo ya kuanzishwa kwake’’.
Aidha, dokta Ndugulile ameenda
mbali zaidi kwa kusema baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakijishughulisha pia na masuala yanayoenda kinyume na maadili ya Tanzania
hivyo amaitaka idara hiyo ihakikishe kila shirika lisilo la kiserikali linatumia
fedha inazopatiwa kwa malengo
yaliyokusudiwa.
Akizungumzia suala la huduma za
jamii kwa wazee, Dk Ndugulile alisema, pamoja na jitihada zinazofanyika katika
kuwahudumia wazee bado eneo hilo lina changamoto kubwa hususan katika misamaha ya kuhudumia wazee katika huduma za afya pamoja na nyumba za kuwatunza
wazee.
Alisema katika vituo vya
kuhifadhia wazee kumekuwa na changaomoto nyingi na wakati mwingine kulazimu
vituo hivyo kusaidiwa na watu wengine
tofauti na idara husika katika huduma mbalimbali kama vile huduma za umeme.
Aidha, ameshauri kupitiwa upya
kwa Sera, Sheria na Miongozo ya Idara kuu ya maendeleo ya jamii kwa kuwa sera
Sheria na miongozi iliyopo haendanane na wakati uliopo sasa.
Amewataka watumishi wa Idara
Kuu ya Maendeleo ya Jamii kuwa wabunifu kwa rasilimali chache zilizopo na
kufanya tafiti wakati wa kufanya kazi zao na kusisitiza kuwa asingependa
watumishi watofautiane naye katika ufuatiliaje wa shughuli za Wizara.
Hivi karibuni Wizara ya Afya
kupitia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii iliendesha zoezi la la kuhakiki
mashirika yasiyo ya kiserikali kwa lengo la kuhuisha orodha ya mashirika hayo
na kuboresha kanzi data ili kupima utekelezaji wa majukumu ya mashirika hayo.








0 Comments