Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye
pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo
amewapongeza wananchi wa kisarawe kwa ushirikiano mkubwa katika ujenzi
wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, Ofisi za walimu,
nyumba, pamoja na vyoo.
Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa
akikagua mradi ya ujenzi wa madarasa wilayani kisarawe katika vijiji
vya Mitengwe, Kitonga, Boga, na kwala.
Katika vijiji hivyo, Jafo alikagua
ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 15, Ofisi za walimu 4, pamoja na
matundu ya vyoo 40 ambapo ujenzi wake unafanyika kwa bora unaotakiwa.
Kutokana na mwamko mkubwa
ulioonyeshwa na wananchi hao katika kushirikiana na serikali na viongozi
walio wachagua akiwemo mbunge na madiwani wote wa kisarawe, Jafo
amesisitiza wananchi wengine katika wilaya mbalimbali kushirikiana na
serikali pamoja na viongozi wao ili kujiletea maendeleo.

0 Comments