Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na
uzalishaji, Christophe Bazivamo
(katikati mbele) akifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya
Timu ya Wataalam kutoka Tanzania wakifuatilia kikao cha Majadiliano upande wa
umeme katika wa 12 wa Baraza la Kisekta
la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baadhi ya Timu
ya Wataalam kutoka nchini Uganda wakifuatilia kikao cha Majadiliano upande wa
umeme katika wa 12 wa Baraza la Kisekta
la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baadhi ya
Timu ya Wataalam kutoka nchini Kenya
wakifuatilia kikao cha Majadiliano upande wa umeme katika wa 12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baadhi ya
Wataalam kutoka nchi mbalimbali wakijadiliana masuala yanayohusu umeme
Baadhi ya
Wataala kutoka Tanzania wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha Majadiliano
kuhusu Nishati Jadidifu wakati wa wa
12 wa Baraza la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Baadhi ya
Wataalam kutoka nchi mbalimbali wakijadiliana masuala yanayohusu Gesi Asilia na Mafuta.
Na Asteria Muhozya,
Arusha
Nchi Washiriki wa Mkutano wa 12 wa Baraza la
Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki wametakiwa kuongeza kasi ya
upatikanaji Nishati miongoni mwa nchi hizo ili kuwezesha Mapinduzi ya Viwanda
na kukuza uzalishaji wa ndani.
Hayo yamesemwa leo la Naibu Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki upande wa Sekta za Kijamii na Uzalishaji, Christophe Bazivamo wakati akifungua Mkutano
huo kwa upande wa Timu ya Wataalam
kutoka nchi za Tanzania, Uganda, Rwanda, Uganda na Kenya.
Bazivamo ameeleza kuwa, ili nchi
hizo ziweze kuendelea Kiviwanda zinahitaji kuwa na nishati ambayo ndiyo kichocheo kikuu cha maendeleo na
kwamba nishati ni miongoni mwa maeneo ya kipaumbele kwa Jumuiya hiyo.
Ameongeza kuwa, bado jamii kubwa
ya wananchi wa Jumuiya hiyo hawajaunganishwa na nishati ya umeme na kuongeza kuwa, ukosefu wa nishati
ya umeme hauzuii tu maendeleo ya kiviwanda bali pia unadidimiza maendeleo ya
watu.
Pia, ameongeza kuwa, mbali na
kudidimiza maendeleo ya watu pia unaathiri sekta ya elimu kwa kuwa, kukosekana
na nishati kunasababisha wanafunzi hususani waishio vijijini kutumia muda
mwingi kutafuta nishati ya kuni kwa ajili ya kupikia badala ya kujikita na
masomo.
Aidha, ameeleza kuwa, matumizi ya
muda mrefu ya kuni kwa ajili ya kupikia pia yanachangia kuathiri afya za kina mama wengi
kutokana na moshi unaotokana na matumizi hayo.
Mkutano huo wa 12 wa Baraza la
Kisekta pamoja na mambo mengine unatarajiwa kujadili maeneo mbalimbali katika
Sekta ya Nishati ikiwemo umeme, Nishati Jadidifu, Gesi na Mafuta.
Mkutano huo ulioanza leo tarehe 30 Oktoba,2017, unatanguliwa na
Timu za Wataalam katika Sekta ya Nishati kutoka nchi husika . Baada ya mkutano
wa Wataalam utafuatiwa na mkutano wa Makatibu
Wakuu kutoka nchi hizo na
kuhitimishwa tarehe 3
Novemba,2017 na Mawaziri wa Nishati wa
nchi husika.
Tanzania inawakilishwa na Wataalam wa masuala ya Nishati
kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Wakala wa
Nishati Vijijini (REA), Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na
Wataalam kutoka upande wa Zanzibar.







0 Comments