Mkurugenzi Mkuu wa Sproxili
Afrika, Chinedum Chijioke akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampuni ya Sproxil inayoongoza duniani, inayotumia teknolojia ya simu za mikononi kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akiishukuru Kampuni ya Sproxil mara baada ya kuzinduliwa.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI) Dr.Samuel Nyantahe akitoa mada yake wakati wa uzinduzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Home of Events, Bw. Anthony Luvanda akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Mmoja wa washiriki akichangia mada.
Wachangia mada.
Majadiliano yakiendelea.
Washiriki wakishuhudia uzinduzi huo.
Kampuni ya Sproxil inayoongoza dunian, inayotumia
teknolojia ya simu za mikononi kudhibiti bidhaa bandia na kumlinda mteja,
imezinduliwa nchini Tanzania.
Sproxil Tanzania inayowezeshwa na mfuko wa
maendeleo ya ubunifu wa bidhaa za binadamu duniani (Human Development
Innovation Fund (HDIF), imewasilisha ubunifu bora wa namna ya kudhibiti bidhaa
bandia/ batili kwa makampuni, taasisi, za udhibiti, serikali na kuwezesha
majadiliano ya wazi kwa ushirikiano wa karibu ili kudhibiti bidhaa bandia.
Majadiliano hayo yamefanyika leo Oktoba 26,
2017 jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency na kuhudhuriwa na wawakilishi
kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, TFDA, TBS, Tume ya Ushindani, Wafanyabiashara
na wadau wengine kutoka sehemu mbalimbali pamoja na waandishi wa habari.
Licha ya kuzindua
huduma ya udhibiti wa bidhaa batili ili
kulinda makampuni ya Tanzania, vilevile
Sproxil inachukua fursa hii kama
jukwaa maalumu kuweka wazi na kueleza
ushirikiano kati ya wadau wote katika suala zima la udhibiti wa bidhaa bandia
na nafasi ya watumiaji wa bidhaa hizo.
Aidha,
kuwasilisha taasisi za kudhibiti na kutakuwa na zoezi la kuthibitisha ubora wa bidhaa chini ya usimamizi wa Bodi ya Viwango
vya Ubora Tanzania (Tanzania Bureau of Standards), na ile ya bodi ya utawala wa
bidhaa za chakula na udhibiti wa madawa nchini Tanzania (Tanzanian Food &
Drug Administration ) na jopo la wawakilishiwa wa sheria, wakurugenzi, kutoka
sekta binafsi waliochaguliwa kuwasilisha matakwa ya sekta binafsi kwa ujumla
wake.
Akizungumzia
umuhimu wa uzinduzi huu kwa jamii ya Watanzania kwa ujumla, Mkurugenzi Mkuu wa
Sproxili Afrika, Chinedum Chijioke alisema;
“Bidhaa
bandia, batili, haramu au zilizo chini ya kiwango ni hatari kwa afya za
watumiaji wasio na hatia, upotoshaji wa ubora wa bidhaa na pia zinateremsha
ubora na mwelekeo wa kiuchumi.
Uwepo
wa bidhaa bandia na zisizo na sifa zinaathiri vibaya watumiaji na kuathiri sifa
za wazilishaji ndiyo sababu imekuwa wajibu wa serikali na sekta binafsi
kuwawezesha Watanzania kutumia njia bora au zilizo chini ya udhibiti
zinazoratibiwa na Kampuni ya Sproxil."
Kwa
upande wake, David McGinty ambaye ni nahodha wa timu ya HDIF Tanzania amesema;
"Teknolojia
ya kumlinda mteja ya Sroxil ni nzuri na ni mfano bora wa ubunifu, ina vipimo
sahihi na ina ubora wa mawasiliano
(1CT4D) ambayo tunaamini inaweza kufanikisha malengo yaliyokusudiwa kwa
jamii ya watumiaji bidhaaa."
Udhibiti
wa ubora wa bidhaa kwa wataalam wa Sproxil unaweza kutumiwa na bidhaa kutoka
sekta yoyote kwa kutumia simu, Watanzania sasa wanaweza kudhibiti na kupima
ubora wa bidhaa kwa muda mfupi kwa kutumia ujumbe mfupi wakitumia namba maalum
kwenda kwenye vifaa maalum vilivyo katika mtandao wa Sproxil kuhoji na
kuthibitisha haraka ubora wa bidhaa.
Tangu
huduma hii ya udhibiti ubora ilipozinduliwa mwaka 2010, Sproxil imeweza
kudhibiti zaidi ya bidhaa milioni 50 kupitia wateja waliohoji ubora wake
duniani kote na hii ni idadi kubwa kabisa ya kesi hizi kuripotiwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika majadiliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye alisema anaikaribisha Kampuni ya
Sproxil nchini kwani ni fursa ya pekee kwa walaji itakayowawezesha kutumia simu
zao za kiganjani kubaini bidhaa bandia zikiwemo mbegu na mbolea kwani huko
ndiko kuna mbegu feki nyingi.
"Mimi
naona ni fursa ambayo imekuja kwa Watanzania itakayotusaidia na watakaoumia ni
wale wanaotengeneza vitu feki, nawakaribisha sana kwa uwekezaji wao ambao una
faida kwetu," alisema Simbeye.
Kuhusu Sproxil
Sproxil® inatumia
tekinolojia ya simu na ugunduzi wa uhalifu kudhibiti udanganyifu
ili kuthibitisha ubora wa bidhaa ambazo zitawafaa wateja duniani kote.
Ufumbuzi wa bidhaa bora unaotumiwa
na Sproxil umekuwa ukitumiwa na watenegnezaji bidhaa wa kimataifa na bidhaa
bora katika viwanda vyote kudhibiti usambazaji wa bidhaa haramu, kusambaza
taarifa za kweli kwa bidhaa halali na bora, na utumiaji wa fedha kwa bidhaa
zilizokusudiwa kununuliwa kwa matumizi muafaka. Ikiwa na timu yake ya wataalamu
waliotapakaa barani Afrika, Asia na Amerika, Sproxil imeweza kufanya kazi kwa
ufanisi katika mabara yote matano na kutoa huduma kwa zaidi ya nchi 100 duniani
kote. Sproxil ni kampuni pekee inayojali mteja na kulinda bidhaa chini ya ISO
9001 na vyeti vya ubora vinavyotolewa na ISO 27001. Kwa maelezo zaidi na
bidhaa za Sproxil, tafadhali tembelea tovuti ya www.sproxil.com.
0 Comments