Random Posts

Kipa Claudio Bravo apangua penati na kuipeleka Man City robo fainali

 Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Alfred N'Diaye
 Sergio Aguero akishangilia baada ya kutumbukiza golini mpira wa penati 
Kipa Claudio Bravo ameibuka kuwa shujaa wa Manchester City katika mchezo wa jana dhidi ya Wolves baada ya kupangua mikwaju ya penati na kutinga robo fainali ya kombe la Carabao.

Bravo, aliyeokoa michomo mitatu katika muda wa kawaida aliongeza kuonyesha ushujaa wake kwa kupangua penati za Alfred N'Diaye na Conor Coady baada ya mchezo kuisha kwa sare tasa.


Manchester City ilifunga penati zote nne huku, Sergio Aguero kumalizia kiufundi penati ya nne na kufanya matokeo kuwa 4-1.

Post a Comment

0 Comments