Na
Mwandishi Wetu Dar es salaam
Chama
Cha Marafiki wa Oljoro (MAO) wametoa msaada wa vitu mbalimbali wenye thamani ya
shilingi milioni 6 katika Chama cha Kulea Watoto Mayatima(CHAKUWAMA) kilichopo
jijini Dar es salaam.
Akiongea
na Waandishi wa habari wakati wa kukabidhi misaada hiyo leo jijini Dar es
salaam Mwenyekiti wa MAO Bw. Walter Chipeta amesema kuwa wameamua kufanya hivyo
ili kuwafariji watoto hao na kuwajengea maisha yenye furaha.
“Tumeamua
kuja kutembelea na kutoa misaada kwa watoto wetu waishio katika kituo hiki ili
kusaidia kutimiza malengo ya watoto wetu pamoja na kuazimisha kumbukumbu ya
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” alisema Bw. Chipeta.
Kwa
upande wake Mratibu wa Tukio hilo kutoka MAO Bi. Pamela Lwakabare amesema kuwa
msaada iliyotolewa ni pamoja na Vyakula na matunda,vifaa vya michezo ya
watoto,mavazi,vyombo vya chakula ,vifa vya usafi na vinywaji amabvyo vina
thamani ya takribani shilingi milioni 6.
Naye
katibu Mtendaji wa CHAKUWAMA Bw. Hassan Hamis amesema kuwa anashukuru kwa msada
huo kwani imepunguza gharama ya mahitaji kwa watoto wapatao 64 katika
kujikimu kila siku.
Mbali na hayo Mtoto
anayeishi katika kituo hiko Nasiim Kasmal (11) amempongeza Rais wa awamu ya
tano Dkt. Pombe John Magufuli kwa kuanzisha elimu bure kwani imewarahisishia
watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata elimu kwa urahisi
Mwenyekiti wa chama cha Marafiki wa Oljoro (MAO) Bw. Walter
Chipeta kushoto akimkabidhi msaada wa
vitu mbalimbali vyenye mahitaji muhimu kwa katibu mtendaji wa Chama cha Kulea
Watoto Mayatima (CHAKUWAMA) Bw. Hassan Hamis kulia leo jijini Dar es salaam.
Wanachama
wa chama cha Marafiki wa Oljoro (MAO) wakiwa kwenye
picha ya pamoja na baahi ya watoto
wanaoishi katika Chama cha Kulea Watoto Mayatima (CHAKUWAMA) wakati
walipotembelea watoto ha oleo jijini Dar es salaam.


0 Comments