Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini
Anthony Mavunde akizungumza katika mkutano Mkuu wa uchaguzi CCM wilaya ya
Dodoma mjini.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi
CCM wilaya waliohudhuria
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Dodoma
mjini aliyemaliza muda wake Paulo Luhamo akifungua mkutano Mkuu wa uchaguzi leo.
Mbunge
wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya
Dodoma mjini Christine Mndeme katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa wilaya.
MBUNGE wa Dodoma mjini Anthony
Mavunde ameeleza mikakati iliyopo katika kukifanya Chama cha Mapinduzi(CCM)
wilaya ya Dodoma kiweze kujitegemea kuwa ni mpango wa ujenzi wa jengo la
ghorofa nane ambalo litakuwa jibu katika kuinua uchumi.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa uchaguzi
leo uliofanyika katika Ukumbi wa Kikwete Hall wilayani Dodoma, Mavunde amesema
pamoja na mpango huo ni vyema wana CCM wakawa na umoja.
Aidha amewataka kuendeleza mbegu
inayoachwa na viongozi wanaomaliza muda wao kwa kufanya kazi kwa umoja,upendo
na mshikamano ili hatimaye matunda mazuri ya mbegu iliyopandwa yaweze
kuonekana.
“Ndugu zangu tukimaliza uchaguzi mmoja ni mwanzo wa
uchaguzi mwingine na ukitaka kushinda lazima uwe na mpango wa kisiasa
kwak ufanya mikutano ngazi ya kata na katika hili mimi kama mbunge kuanzia
mwakani nitagawa vipasa sauti vitatu na spika za kusimama kwa kila kata ili
kuwezesha kufanyika mikutano hiyo na baadae nitaangalia suala la usafiri,”amesema
Mavunde.
Amewaomba wajumbe wa mkutano huo kuendelea kumshukuru na kumpongeza
Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kuivunja mamlaka ya ustawishaji makao
makuu(CDA) ambayo ilikuwa ni kilio cha wakazi wa Dodoma na kuifanya Dodoma kuwa
makao makuu ya nchi.
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda
wake wilaya ya Dodoma mjini Paulo Luhamo amewataka wajumbe kuzingatia maagizo
ya chama kwa kutochagua mtu kwa ajili ya ukabila,dini wala rangi.
“WanaCCM wenzangu
chagueni kiongozi atakayetoka ndani ya CCM na sio nje ya CCM,atakayefanyia kazi
maamuzi ya CCM,na mimi pamoja na kwamba nitakuwa nje ya uongozi nitashirikiana
na uongozi mpya usiku na mchana,mvua na jua ili kulinda heshima ya Dodoma kuwa
makao makuu ya Chama na Serikali,”amesisitiza Luhamo.
Amewataka wana CCM kuachana na utaratibu waliokuwa nao wa
kubadilisha mbunge kila baada ya miaka mitano na badala yake wamempa heshima Rais
kwa kuendelea kumchagua Mavunde kama mbunge wao,kumlinda na kumuombea.
“Mbunge wetu anafanya kazi kubwa kwa ajili ya CCM,sisi
tumekuwa na utaratibu wa kuleta mbunge kila baada ya miaka mitano tuache
utaratibu huu,rais ametupa heshima ya kumchagua Mbunge wetu katika baraza la
mawaziri heshima ambayo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1975,hivyo kama rais
ametupa heshima hiyo nasi tuilinde,”amesema Luhamo.
Wagombea wanaogombea nafasi ya
Mwenyekiti ni pamoja na Adam Msendo, Stephen Mwanga na Robert Mwinje.





0 Comments