Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa namba maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi. Wanaoshuhudia kulia kwake ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Godfrey Simbeye. Kushoto kwa Mhagama ni Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Khamis Mwinyimvua.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akifurahia pamoja na viongozi wenzake mara baada ya uzinduzi huo.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 660 Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo akimkabidhi hundi ya sh. milioni
200 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera ( kulia) kwa ajili ya ujenzi wa
kituo cha afya Mererani.
Mwenyekiti
wa bodi wa mfuko, Godfrey Simbeye akizungumza kabla ya uzinduzi wa namba hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko akizungumza kwenye tukio hilo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama akitoa hotuba katika tukio hilo.
Waziri wa Afya,
Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akisisitiza jambo baada ya kukabidhiwa
hundi yake.
Washiriki
wakifuatilia mkutano huo.
Mawaziri
wakiangalia namna ya kutuma fedha kwa kutumia namba 0684909090 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa
udhamini wa kudhibiti Ukimwi. Aliyesimama ni Mkuu wa kitengo cha sheria wa
TACAIDS, Elizabeth Kaganda.
Waziri Mhagama (katikati) akiwa katika picha na viongozi wengine.
Picha zote na Philemon Solomon
Na Julian Msacky-Nchi yangu Blog.
TUME ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS), imezindua rasmi namba maalumu ya kuchangia Mfuko wa
Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.
Uzinduzi huo umefanyika
Dar es Salaam Oktoba 21, 2017 na kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama.
Mhagama alitaja namba ya
uchangiaji wa mfuko huo kuwa ni 0684909090 na kwamba kila mwananchi anahimizwa
kuchangia ili fedha itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi Vya
Ukimwi.
"Leo ni siku maalumu
kwa nchi yetu...inaonesha tumeanza kujitegemea kupitia mfuko huu wa udhamini
katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi," alisema.
Waziri alisema mfuko huo
umeanzishwa kwa Sheria Namba 6 ya Mwaka 2015 na utakuwa unachangiwa na
Watanzania wenyewe.
"Huu ni mfuko wa umma
na tunabeba jukumu hilo kama Serikali na lengo kuu ni kuwahudumia Watu wenye
maambukizi," alibainisha.
Alisema fedha za mfuko huo
zitatumika kununua dawa za septrine ambazo ni maalumu kwa ajili ya kufubaza
Virusi Vya Ukimwi na zitatolewa bure.
Mhagama alisema takwimu
zinaonesha kuna Watanzania milioni 1.4 wanaoishi na VVU na watu 48,000
huambukizwa virusi hivyo kila mwaka nchini.
"Kati ya WAVIU
milioni 1.4 wanaotumia dawa ni laki 8, Watanzania kati ya laki 4 hadi 5
hawatumii dawa, hivyo tupunguze utegemezi angalau kwa asilimia 40 ili kudhibiti
Ukimwi," alifafanua.
Pamoja na hali kuwa hivyo,
Waziri alisema asilimia 94.7 ya Watanzania hawana VVU na Ukimwi na wanahitaji
kulindwa ili waendelee kubaki salama.
Alisema kulingana na
Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (2013/14-2017/18) uliothaminishwa,
mahitaji ya taifa ya kugharimia mwitikio wa Ukimwi katika kipindi cha miaka
mitano yanakadiriwa kufikia sh. trilioni 6.
"Asilimia 93 ya fedha
hizi zinatarajiwa kutoka kwa wafadhili na asilimia 7 kutoka vyanzo vya ndani.
Sehemu kubwa asilimia 56 ya fedha zote katika miaka hiyo ni kwa ajili ya
kununua dawa," alisisitiza.
Katika hatua nyingine,
Mhagama alikabidhi hundi ya sh. milioni 660 kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa ajili ya kununua dawa aina ya
cotrimoxazole za watu wanaoishi na VVU.
Pia alikabidhi hundi ya
sh. milioni 200 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera ili kujenga kituo
cha afya Mererani ikiwa ni kuunga mkono ahadi ya Rais John Magufuli kusaidia
ujenzi wa kituo hicho.
Viongozi wengine
walioshiriki tukio hilo la uzinduzi ni Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, DK
Leonard Maboko na Mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo, Godfrey Simbeye.
Habari hii imeandaliwa na
blog ya NCHI YANGU. Simu 0718981221














0 Comments