Random Posts

Semina endelevu ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kufanyika Oktoba 12-13 2017 mlimani city jijini Dar es salaam.

Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, QS Albert Munuo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jiji Dar es salaam Oktoba 4, 2017 kuhusiana na maandalizi ya semina endelevu  ya bodi ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi itakayofanyika oktoba 12-13  2017 mlimani city jijini Dar es salaam (kulia) Afisa Mkuu Ukaguzi wa Ndani wa Bodi hiyo, Ezekiel Stephen, na kushoto Mwanasheria wa Bodi, Ibrahim Mohamed. 
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, QS Albert Munuo (kushoto katikati) akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusiana na maandalizi ya semina endelevu  ya bodi ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi itakayofanyika oktoba 12-13  2017 mlimani city jijini Dar es salaam (wakwanza kulia) Afisa Mkuu Usajili wa Bodi hiyo, Mashaka Bundala.
Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, QS Albert Munuo (kulia katikati) akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari wakati akielezea kuhusiana na maandalizi ya semina endelevu  ya bodi ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi itakayofanyika oktoba 12-13  2017 mlimani city jijini Dar es salaam.
.....
Waziri wa Ujenzi uchukuzi na mawasiliano professa Makame mbarawa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye semina endelevu  ya bodi ya Usajili wa wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi itakayofanyika oktoba 12-13  2017 mlimani city jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kaimu msajili wa bodi hiyo Albert Munuo amesemakuwa semina hiyo inalenga kuwapa frusa wataalamu katika sekta ya ujenzi kupata nasaha kutoka Kwa viongozi wa serekali na kubadilishana uzoefu wa kazi za kitaalamu kwa lengo la kuziboresha.

Aidha ameongeza kuwa semina hiyo pia itawanoa wabunifu majengo,  wasanifu wa ndani ya majengo,  wabunifu wa mandhari ya nje, wakadiriaji majenzi, wasimamizi ujenzi, watathimini majengo na wadau wengine katika sekta ya ujenzi ili kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika sekta ya ujenzi.

Sanjari na hayo Bw.Munuo amesema semina hiyo itakuwa na mada mbalimbali ikiwemo mbinu za kupunguza madhara ya matetemeko ya ardhi, ukaguzi wa miradi ya ujenzi pamoja na matengenezo ya majengo na miundombinu katika sekta ya ujenzi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wadau wa sekta ya ujenzi ikiwemo wahandisi, wakadiriaji majenzi na wabunifu majengo kuhudhuria kwa wingi kwenye semina hiyo ili kuongeza ujuzi na maarifa ya kuboresha utendaji kazi wao. 

Post a Comment

0 Comments