Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwasisitiza watumishi
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanafanyakazi
kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali ya kukusanya Shilingi
trilioni 17.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza na
baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga kuhusu
kufanya juhudi ya kukusanya mapato ili azma ya Serikali ya kuwahudumia wananchi
kikamilifu itimie.
Meneja
wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Shinyanga, Bw. Jumbe Samson (aliyesimama)
akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya Mkoa wake
kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya
ziara ya kikazi katika mkoa huo.
Baadhi
ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga wakimsikiliza
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa
akizungumzia umuhimu wa watumishi wa Mamlaka hayo kote nchini kuzingatia maadili ya kazi zao, alipofanya ziara ya
kikazi katika mkoa huo
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (aliyesimama)
akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga
kuhusu nia ya Serikali katika kuhakikisha kodi ya majengo na mabango
inakusanywa kikamilifu kwa manufaa ya wananchi na Taifa, alipofanya ziara ya
kikazi katika mkoa huo
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi na watumishi wengine wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa
wa Shinyanga, alipofanya ziara ya kikazi kukagua namna Mamlaka hayo
inavyokusanya kodi.
Meneja
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Bw. Jumbe Samson (aliyesimama)
akimweleza Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto) mikakati ya mkoa wake
katika kuhakikisha mapato yanaongezeka.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny
Mwaipaja, Shinyanga
Serikali
inatarajia kuajiri wafanyakazi 400 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika
kipindi kifupi kijacho ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa watumishi
katika Mamlaka hayo, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi na makusanyo ya kodi.
Ahadi
hiyo imetolewa Mjini Shinyanga na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji, wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji wa Mamlaka hayo mkoani
humo.
Dkt.
Kijaji amesema kuwa taratibu zote zimekamilika na wakati wowote nafasi za ajira
zitatangazwa na kwamba nafasi hizo zimelenga kuiwezesha TRA kuwafikia watu
wengi zaidi na kuongeza wigo wa makusanyo ya kodi.
“Tunatambua
changamoto ya uchache wa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ndio maana
tumeamua kuajiri wafanyakazi hao 400 ambao ni wengi kuliko kada nyingine ili
tuweze kuimarisha utendajikazi wa Mamlaka na hivyo kuongeza makusanyo ya kodi
zinazotakiwa kwa shughuli za maendeleo nchini” alisema Dkt. Kijaji
Alisema
kuwa pamoja na uhaba wa watumishi, anaamini kuwa lengo la mwaka huu la
kukusanya shilingi trilioni 17 ambazo Mamlaka hayo imepangiwa yatafikiwa na
ikiwezekana kuzidi kwa kutumia wafanyakazi waliopo.
Dkt.
Kijaji alitoa rai kwa wafanyakazi wa TRA kuwa waadilifu na kwamba
atakayebainika kukiuka maadili yake ya kazi atachukuliwa hatua kali za
kinidhamu na kisheria.
Awali
Meneja wa Mamlaka ya Mapato mkoa wa Shinyanga Bw. Jumbe Samson, alieleza kuwa
mkoa wake umepangiwa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 18 na kwamba wanauhakika
wa kufikia lengo hilo kutokana na mikakati mbalimbali waliyojipangia ikiwemo
kusimamia ukusanyaji kodi kikamilifu katika sekta ya madini.
Kwa
upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Bw. Beatus
Nchota alisema kuwa Mamlaka yake imejiwekea mipango ya kufungua ofisi zake kila
wilaya hapa nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza wigo wa
ukusanyaji wa mapato ya Serikali ili lengo walilopewa la kukusanya shilingi
trilioni 17 liweze kufikiwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Josephine Matiro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
mkoa wa Shinyanga, alisema kuwa Serikali mkoani humo itahakikisha kuwa TRA
inatimiza malengo yake ya kukusanya kodi na kumhakikishia Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwamba watasimamia kikamilifu ukusanyaji wa
mapato ya Serikali.







0 Comments