Mkuu wa Wilaya
ya Gairo Mkoani Morogoro Bi. Siriel Mchembe akieleza mikakati iliyosaidia
Wilaya hiyo kuongeza kiwango cha ufaulu hadi kufikia asilimia zaidi ya 70 mwaka
huu kwa Shule za msingi wakati wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu walipomtembelea
Ofisini kwake ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa Tume hiyo wanapotembelea Ofisi za watendaji wa Tume hiyo ngazi ya Wilaya.
Afisa Utumishi
wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Anyagwe
Lupembe akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu sheria na Kanuni zinazotumika
katika utumishi wa Umma kwa watumishi wa Tume ya utumishi wa Walimu Wilaya ya
Gairo wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tume hiyo.
Mkuu wa Kitengo
cha TEHAMA wa Tume ya utumishi wa Walimu
Bi. Devotha Gabriel akiwasiliosha mada kwa watumishi wa Tume hiyo Wilaya ya
Gairo kuhusu matumizi salama ya vifaa vya TEHAMA pamoja na njia sahihi za
mawasilisno kwa njia ya mtandao.
Mkuu wa Wilaya
ya Gairo Mkoani Morogoro Bi. Siriel Mchemba (katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Ujumbe wa Tume ya utumishi wa Walimu uliongozwa na Mkuu wa Kitengo
cha TEHAMA wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bi. Devotha Gabriel. Wa kwanza kulia
ni Katibu Tawala wilaya ya Gairo Bw. Adam Bibangaba.
Wajumbe kutoka
Tume ya Utumishi wa Walimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani
Morogoro Bi. Siriel Mchemba wakati walipomtembelea Ofisini kwake.
(Picha zote na Frank Mvungi- Gairo, Morogoro)
.....
Frank Mvungi-MAELEZO-
Gairo, Morogoro
Tume
ya Utumishi wa Walimu imeanza kutekeleza kwa vitendo dhana ya Serikali ya Awamu
ya Tano inayososisitiza uwajibikaji kwa kutoa mafunzo ya TEHAMA na utawala kwa Makatibu
wasaidizi ngazi ya Wilaya ili kuongeza ufanisi na kukuza kiwango cha elimu nchini.
Akizungumza
na Makatibu Wasaidizi wa Wilaya wakati wa kuhitimisha ziara ya Wajumbe wa Tume
hiyo wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Devotha
Gabriel amewasisitiza viongozi hao kuzingatia taaluma ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi.
“Mafunzo
tunayowapa Makatibu Wasaidizi katika Wilaya zote yanalenga kuwajengea uwezo wa
kutumia vifaa vya TEHAMA kwa kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu zote
za Utumishi wa Umma ikizingatiwa eneo mojawapo tunalosisitiza ni kufuata taratibu
za Utumishi wa Umma katika kuwahudumia walimu” Alisisitiza Devotha.
Bi. Devotha amesema
kuwa utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi wa Tume hiyo ngazi ya Wilaya ni utekelezaji
wa moja ya mikakati ya Tume hiyo ili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia walimu
ili waweze kutekeleza majukumu yao
ipasavyo.
Aidha Bi. Devotha alisistiza
kuwa dhamira ya Tume hiyo ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa hivi karibuni na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jafo katika kushughulikia
masuala yote yanayowahusu walimu ndio maana Katibu wa Tume amekuwa akifuatilia
na kuhakikisha maagizo hayo yanatekelezwa kikamilifu.
Utekelezaji wa maagizo
ya Mhe. Wzairi unaenda Sambamba na kushughulikia masuala ya walimu kwa wakati na
kujenga mifumo ya TEHAMA ambayo inawaunganisha Makatibu Wasaidizi katika ngazi
ya Wilaya na Makao Makuu ya Tume hiyo hali itakayorahisha utendaji, kupunguza
gharama,kuokoa muda na kutua changamoto za walimu kwa wakati.
Aidha, Bi. Devotha alitoa
wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia juhudi za Tume ya Utumishi wa
Walimu katika kuimarisha utendaji kazi wa Tume hiyo kwa kujitolea vifaa vya
TEHAMA na kuwajengea uwezo Makatibu Wasaidizi ngazi ya Wilaya.
Kwa upande wake mkuu
wa Wilaya hiyo Bi Bi Siriel Mchembe amesema kuwa Wilaya hiyo imefanikiwa kukuza
kiwango cha elimu hadi kufikia zaidi ya asilimia 70 ya ufaulu katika matokeo ya
Darasa la saba.
“Nimefanikiwa
kusimamia kikamilifu ujenzi wa miundo mbinu kama madarasa, vyoo na miundo mbinu
mingine hali ambayo imeongeza na kukuza morali ya walimu katika Wilaya yetu.”
Alisisitiza Mchembe.
Akifafanua Mchembe
amesema maendeleo ya sekta ya elimu katika Wilaya yake ni Kipaumbele na ameweka
utaratibu mzuri wa kusimia utekelezaji wa mikakati ya kukuza elimu Wilayani
humo.
Kwa
upande wake Afisa Utumishi wa Tume hiyo
Bi Anyagwe Lupembe amesema kuwa Tume hiyo imejikita kujenga uwezo kwa watumishi
wake ili watimize majukumu yao kwa kuzingatia sheria Kanuni na taratibu za
Utumishi wa Umma.
Tume
ya Utumishi wa Walimu imekuwa ikitekelza mpango wa kuwajengea uwezo Makatibu
wasaidizi katika Wilaya zote nchini na kwa kuanza tayari mpango huo umetekelzwa
katika mikoa ya Dodoma na Morogoro hivyo ni muda muafaka kwa wadau kujitokeza
kuunga mkono juhudi hizo.





0 Comments