KAMPUNI
ya simu nchini TECNO imezindua duka kubwa zaidi la simu za mkononi
“TECNO SMART HUB” lenye ukubwa wa mita za mraba 110, duka hilo lenye
uwezo wa kuhudumia takribani wateja zaidi ya 50 kwa mara moja.
(Meneja Daniel Xu akizindua na kuwakaribisha wadau wa TECNO)
Nia
ya TECNO SMART HUB hii kubwa ni kutoa huduma zote zinazohusu simu za
mikononi za kisasa yaani “smart phones” ikiwemo simu zenyewe na vifaa
vyake kama vile chaja, klabu za watumiaji wa TECNO, nahuduma kwa wateja ya papo kwa papo.
Wakati
wa uzinduzi huo, meneja wa kampuni ya simu za TECNO Bw. Daniel xu,
aliongoza wateja waliofika kushuhudia uzinduzi wa SMART HUB HIYO kukagua
na kujionea uzir wa duka duka hilo jipya huku akitoa maelezo kwa
wageni walioalikwa kazi mbalimbali za vitengo vilivyomo katika duka
hilo, TECNO imezindua duka hili maalumu ili kuwapa wateja wake huduma
bora na za kisasa Zaidi kuwahi kutokea katika ulimwengu wa biashara za
simu za mkononi nchini.
Aidha
wateja pamoja na wageni waalikwa wali furahia kuhudhulia uzinduzi huo
baada ya kupata elimu ya jinsi ya kutunza simu za kisasa “smart phones”
vizuri hasa kwa watumiaji wapya wa simu hizo. Lakini kwa sasa TECNO
wameweza kuweka mafundi wao kwenye TECNO SMART HUB hiyo kubwa, ambapo
pia wanatoa huduma za ushauri pamoja na kutengeneza simu kwa ustadi wa
juu kabisa endapo simu ya mteja itakua na tatizo lolote.
Uzinduzi
wa TECNO SMART HUB, uliendana sambasamba na burudani za aina mbalimbali
ikiwemo muziki na vinywaji vilivyotolewa bure kwa wateja wa TECNO
waliofika katika eneo la tukio.
Kampuni
ya simu za TECNO, ndio kampuni inayo ongoza kwa kutoa simu za kisasa
zenye ubora wa hali ya juu pamoja na huduma bora zaidi, kuliko kampuni
yoyote nchini. Na kupitia duka lao hilo utafurahia ulimwengu wa simu
bora za kisasa uliojaa huduma bora za kujali wateja.
Mwonekano Smart hub:
(Muonekano wa duka jipya la TECNO SMART HUB lililopo Mlimani City)
(Eneo la mapumziko na vipuli/accessories za simu)
(Wateja wakipata maelezo juu ya bidhaa mpya ya SPARK katika duka la TECNO SMART HUB)
(Mteja akipata maelekezo na ufumbuzi kutoka kwa mtoa huduma wa TECNO)
(Sehemu ya duka, eneo la display za simu)
Sehemeu ya wateja kupumzika wakusubiri huduma
0 Comments