Na: Calvin Edward Gwabara Morogoro.
Mtandao wa
Elimu (TEN/MET) kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania wawakutanisha
walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania ili kutafuta mbinu za kukabiliana na
changamoto zinazorudisha nyuma au kukwamisha jitihada zao za kutoa elimu bora
nchini.
Meneja
Miradi wa Mtandao huo, Mwalimu Alistidia Kamugisha (wa kwanza kulia)
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kongamano hilo.
Akizungumza wakati wa utambulisho na lengo la kongamano hilo maalumu
katika siku ya Mwalimu duniani, Afisa miradi ya mtandao huo Mwl.
Alestidia Kamgisha alisema walimu wanachangamoto nyingi ambazo zisipotatuliwa
zitaendelea kushusha ubora wa elimu kutokana na kuporomoka kwa hali ya mwalimu
kufundisha.
“kukutana kwao kwa pamoja kutasaidia kila mmoja kusikia changamoto
na mafanikio ya mwalimu mwenzake kutoka mkoa mwingine lakini pia kujifunza kwa
walimu wengine waliofanikiwa wakiwa ndani ya changamoto hizo”, alisema
Kamugisha.
Pia Afisa Miradi huyo wa mtandao wa elimu Tanzania aliongeza kuwa
mawazo ya pamoja kutoka kwa wadau hao yatasaidia katika kubuni mbinu za pamoja
kama wadau ili kusaidia kutatua chaangamoto hizo na kurudisha nguvu ya
mwalimu katika kufundisha na kufaulisha.
Aidha
akieleza hali ya shule yake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu
Atulinda Musebura alisema kuwa shule yake inawalimu watano tu lakini
inazaidi ya wanafunzi 1000 idadi ambayo ni kubwa sana kwenye uwiano kati ya
mwalimu mmoja na mwanafunzi.
Mwalimu
mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu Atulinda Musebura.
“hali hii inatulazimu kufundisha kwakuelekeza nguvu kwa darasa la saba
ili kuwawezesha wanafunzi hao kufaulu mitihani yao ya mwisho na wanapoondoka
nguvu zetu tunazielekeza kwa darasa la nne ambao nao wanakuwa na mtihani wa
Taifa,
Hali hiyo inawanyima wanafunzi wengine kwenye nyakati Fulani kukosa
masomo na hata kuwatesa walimu hao kwa kufanya kazi kupita uwezo wao na mwalimu
anapopata dharura hali huwa mbaya zaidi kwani walimu hao kila mmoja anavipindi
zaidi ya 67 kwa wiki badala ya 40”,alisema Musebura.
Kwa upande
wake muwezeshaji kwenye kongamano hilo bwana Zelote Loilang’akaki alisema
mkakati wa serikali kutoa elimu bure umesaidia kuwepo kwa ongezeko kubwa la
wanafunzi mashuleni lakini swala la ongezeko la walimu halikuzingatiwa
hivyo kuwafanya walimu kuzidiwa na mzigo wa kazi ya ufundishaji.
Muwezeshaji
wa kongamano hilo Bwana Zelote Loilang’akaki akizungumza na washirki hao.
“Changamoto ya upungufu wa walimu umekuwa mkubwa kwa shule za msingi
wakati wa idadi ya walimu wa Sayansi ikibaki kuwa ndogo kwenye shule za
secondary kwamfano kuna upungufu wa walimu wa Sayansi 64 sekondari wakati
msingi kunaupungufu wa walimu 614 kwa mujibu wa ripoti za TEN/MENT kwa wilaya
ya Mvomero pekee”, alisema Loilang’akaki.
Pia alibainisha kuwa kwa mujibu wa serikali idadi ya walimu
imeongezeka kufika 165,856 mwaka 2010 hadi 2011 hadi kufika 190,957 mwaka
2014 hadi 2015.
Taarifa za chama cha walimu Tanzania (CWT) zinaonyesha nchi inaupungufu
wa walimu 100,000 kwa shule za msingi 500,000 shule za sekondari ambapo walimu
wa Sayansi 30,000 na sanaa 20,000 huku taarifa za elimu ya msingi (BEST 2016)
zinaonyesha upungufu ni walimu 7291 wa hesabu 5118 Biology 5375 kemia 6873
walimu wa fizikia.
Siku ya
walimu duniania mwaka 2017 imebeba ujumbe usemao “mwalimu anastahili mazingira
bora na huru ya kufundishia: kodi anayolipa itumike kwaajili ya kumjengea uwezo
na kuboresha mazingira yake”.
Bwana
Prosper Lubuva Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo (CWT) akiwasilisha mada juu ya
mapendekezo ya Shirika la kazi duniani na ILO na UNESCO kuhusu hali ya walimu
ya mwaka 1966.
Mwalimu akiwa
amefungwa kitambaa na kuagizwa kitu ukumbinu hapo ikiwa ishara ya kuona
changamoto na vikwazo anavyokutana navyo Mwalimu kwenye kufikia malengo
yake ya kufundisha na kufaulisha.
Wadau hao
wakifuatilia mada ya mapendekezo ya hali ya mwalimu duniani.
Baadhi
ya wadau hao wa Elimu wakifuatilia kongamano hilo.
0 Comments