Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
wakiwasili Ruaha -Kware Wilya ya Kilolo Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya
kujionea shamba lenye ekari 3000 kwaajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita Mkakati wa Mtandao
wa Kijani Kibichi Tanzania, Dkt. Kissui Stephen akielezea malengo ya
ziara hiyo (kushoto kwake) Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
pia mwanzilishi wa mtandao huo, Adam ngamange, kulia katikati ni Afisa Mtendaji
Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilya ya Kilolo Mkoa wa Iringa, John Mchopa,
na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Ambapo amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaleta
wakulima waweze kuona mashamba wanaotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kutangaza
mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo.
Alisema kama mtu awezi kulima myenyewe kuna wataalamu
mbao watawekwa shambani kwa garama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.
Pia Dkt.
Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazo zalisha mara tatu zaidi na mbolea
za Organic ambazo hazina madawa na haziharibu aridhi ili
kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahiya.
Alisema pia
wanatanga maswala ya masoko kutokana huu ulimwengu wa masoko yani unaanza
kwanza kutafuta masoko ndipo unaanza kulima.
"Sisi
tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima
kwenye masoko" Alisema Kissui.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
pia mwanzilishi wa mtandao huo, Adam ngamange akielezea miradi ya
kuamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba
kwaajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilya ya Kilolo Mkoa wa
Iringa.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
pia mwanzilishi wa mtandao huo, Adam alisema katika mtandao wanafanya miradi ya
uwamasishaji kilimo na ufugaji kibiashara.
Alisema waligundua watanzania wengi wanalima
lakini sio kibishara ambapo wameanza na miradi mitano katika miradi hiyo kuna
maeneo maalum kama Ruaha ni aridhi yakupata papai iliyokuwa salama kwakuwa watangaza maswala ya kilimo hai.
Aliongeza kuwa mradi huo wenye ekari 384 ambazo
watazigawa katika mafungu ya ekari 32 kila ekari ambazo zitapandwa katika
utaratibu wa kili mwezi mara moja ili waweze kusamba papai kwenye masoko
makubwa.
Wanachama wa Mtandao wa
Kijani Kibichi Tanzania wakitembelea na kukagua shamba kwaajili ya kuwekeza
kilimo cha PAPAI.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita Mkakati wa Mtandao
wa Kijani Kibichi Tanzania, Dkt. Kissui Stephen akimtambulisha Mwenyeji
wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.
Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha
(alienyosha mkono), Amani Matinya akiwaonesha wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
ukumbwa shamba hilo na mbinu zinazotumika kumwagilia.
Muonekano wa shamba hilo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
wakielekea kujionea maji yanayotoka Mto Lukosi unaotumika kwaajili ya kilimo
cha umwagiliaji.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
wakiangalia mashine zinazovuta maji kutoka Mto Lukosi kwajili ya kilimo cha
umwagiliaji.
Muonekano wa Mto Lukosi.
Mmoja wa wakulima wa eneo la Ruaha -Kware Wilya ya Kilolo Mkoa wa Iringa(kulia)
akifafanua jinsi maji yanavyo sambazwa kwa wakulima.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania
wakipanda kwenye basi tayari kuanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam.
HABARI/ PICHA NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG


0 Comments