Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa,
akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Eng. Jackson Masaka pamoja na viongozi
wengine wa wilaya hiyo, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Singida.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi China Henan International Corporation anayejenga daraja
la Sibiti lenye urefu wa mita 82 na barabara za maingilio kwa kiwango cha
changarawe zenye urefu wa KM 25, alipokagua ujenzi wa miradi hiyo mkoani
Singida.
Meneja wa Wakala wa
Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo, akifafanua jambo kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias
Kwandikwa (wa pili kulia), alipokagua ujenzi wa daraja la Sibiti lenye urefu wa
mita 82 na barabara za maingilio kwa kiwango cha changarawe zenye urefu wa KM
25, mkoani Singida.
Mhandisi Mshauri Mr.
Sunil Singh, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta
ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa, uwekaji zege katika moja ya boksi kalvati
kubwa linalojengwa katika barabara za maingilio ya daraja la Sibiti, mkoani
Singida.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa
(katikati), akioneshwa na Mhandisi Mshauri Mr. Sunil Singh (kulia), nguzo
zilizojengwa kushikilia daraja la sibiti, alipokagua ujenzi wake jana, mkoani
Singida. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida
Eng. Leonard Kapongo.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mhe. Elias Kwandikwa,
akizungumza na wananchi wa kata ya Mpambala wilayani Mkalama, wakati alipokagua
ujenzi wa daraja la Sibiti lenye urefu wa mita 82 na barabara za maingilio kwa
kiwango cha changarawe zenye urefu wa KM 25, mkoani Singida.
Muonekano wa nguzo tatu zitakazoshikilia Daraja la Mto Sibiti lenye
urefu wa Mita 82 na upana wa mita 10.5. Daraja hilo ni kiungo muhimu kwani litaunganisha
Wilaya ya Iramba na Mkalama mkoani Singida na Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Mheshimiwa Elias Kwandikwa
(Mb), ameyataka makampuni yanayopewa kazi na Serikali ya kusanifu ujenzi wa barabara
kufanya kazi hiyo kwa umakini kwa kutambua na kubainisha changamoto
zitakazosababisha ucheleweshaji wa ujenzi wa miundombinu hiyo hapa nchini.
Mhe. Kwandikwa
ametoa maelekezo hayo wakati akikagua ujenzi wa Daraja la Mto Sibiti na barabara za maingilio kwa kiwango cha changarawe
mkoani Singida na kusisitiza kuwa wasanifu barabara wakifanya kazi kwa weledi
kutasaidia Serikali kuweza kuepukana na usumbufu, ongezeko la gharama na
ucheleweshwaji wa miradi hiyo.
"Changamoto
za barabara ni zile zile katika maeneo mengi hivyo wasanifu waongeze weledi ili
kusaidia mkandarasi kufanya kazi zake kwa wakati na haraka na hivyo kusaidia
Serikali kutopoteza fedha kwa miradi mingi inayochukua muda mrefu",
amesisitiza Mhe. Kwandikwa.
Amezitaja
changamoto ambazo zimesababisha ucheleweshwaji wa ujenzi wa daraja la sibiti na
barabara za maingilio ikiwa ni ukutaji wa mawe mengi katika barabara hiyo na
ongezeko wa makalvati ambapo hapo kwenye usanifu wa awali havikuwepo.
Aidha amemtaka
mkandarasi China Henan International Corporation anayejenga daraja hilo
kuongeza vifaa eneo la kazi ili kuongeza kasi ya ujenzi na kumaliza kwa muda
uliopangwa.
Mhe. Kwandikwa
amewatoa hofu wananchi wa mikoa ya Simiyu na Singida wanaounganishwa na daraja
hilo kuwa mradi huo utakamilika mapema mwanzon mwakani.
"Mradi huu
ni ukombozi katika kukuza uchumi wa mikoa hii, hivyo Serikali inajitahidi kila
linalowezekana kuhakikisha unakamilika kwa wakati", amesema Mhe.
Kwandikwa.
Kwa upande wake
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Eng. Leonard Kapongo,
amemhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wataendelea kumsimamia mkandarasi
kikamilifu ili mradi ukamilike kwa wakati viwango vilivyokubaliwa katika
mkataba.
"Maendeleo
ya mradi mpaka sasa unaendelea vizuri na kazi zilizobaki ni uwekaji wa vyuma
juu ya nguzo za daraja ambapo utakamilika hivi karibun", amesema Eng.
Kapongo.
Ujenzi wa
daraja la sibiti lenye urefu wa mita 82 na upana wa mita 10.5 linalounganisha
wilaya Mkalama na Meatu utahusisha na ujenzi wa barabara za maingilio zenye
urefu wa kilomita 25 unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwakani na utagharimu
kiasi cha shilingi bilioni 18.1 ambazo zote zinagharamiwa na Serikali ya
Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano







0 Comments