Random Posts

Watoto 28 wafanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

 Madaktari bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  na wenzao wa Shirika la  Mending Kids  la nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua na kuziba tundu la moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji  kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
 Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Shirika la  Mending Kids  la nchini marekani wakimfanyia mgonjwa  upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Catheterization) na kuzibua mishipa ya Moyo katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo . Jumla ya watoto 28 wamefanyiwa upasuaji  kati ya hao 19 upasuaji wa bila kufungua kifua na tisa upasuaji wa kufungua kifua.
 Afisa Muuguzi wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Veronica Vedastus na Arianna Minghetti  wa Shirika la Mending Kids  la nchini Marekani  wakimnywesha maziwa mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo  bila ya kufungua kifua (Catheterization) katika kambi maalum ya siku tano ya upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa  na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.
Maafisa Uuguzi  wa chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwezao wa  Shirika la  Mending Kids  la nchini Marekani  wakijadiliana kuhusu maendeleo ya wagonjwa waliolazwa katika chumba hicho baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya siku tano ya  upasuaji kwa watoto inayofanyika katika Taasisi hiyo. Watoto wanaofanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ni wale waliozaliwa  na magonjwa ya moyo kuwa na tundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri.
Picha na JKCI

Post a Comment

0 Comments