Na Tiganya Vincent RS-Tabora
Vijana Mkoani Tabora wametakiwa kuacha tabia ya kukaa vijiweni na kusikiliza maneno ambayo hayawasaidia kuwafundisha namna ya kupata maendeleo badala yake waatumie muda kujiari katika uzalishaji wa pamba na mazao mengine yatakawasaidia kujipata kipato na kuinua maisha yao.
Kauli hiyo imetolewa jana katika maeneo mbalimbali ya Kata za Wilaya ya Kaliua na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa zoezi uhamasishaji wa kilimo cha zao la Pamba kisasa.
Alisema kuwa ni vijana Mkoani humo wakatumia kipindi hiki cha msimu wa mvua kilichoanza kwenda mashambani na kulima pamba kisasa ili waweze kuzalisha kwa wingi na ubora , hatimaye waweze kupata pesa nyingi zitakazowasaidia kuinua maisha yao na kuondokana na umaskini.
Mwanri alisema kuwa vitendo vya baadhi ya vijana kukaa vijiweni na kusikiliza ushauri wa wenzao ambao wameshindwa maisha kwa sababu ya kushindwa kujituma ndio wao wa kwanza kulalamikia tatizo la ukosefu wa ajira, wakati fursa zipo kwenye maeneo yao kupitia sekta ya kilimo na ufugaji kisasa.
Alisema kuwa marafiki wa vijana ambao hawapi ushauri mzuri wa kujiletea maendeleo badala yake ni kuwajaza maneno ya kipuuzi hawafai kuwa marafiki zao na ni vema wakawaepuka.
“Mimi nimekuja kuwafundisha jinsi ya kupata utajiri kupitia pamba…kwa maana nyingine hivi sasa ninaongea na mamilioni wangu wajao…uwe na Imani kuwa ukilima kwa kuzingatia maelekezo niliyokufundisha na kwa kuzingatia ile Sheria ya Pamba na kanuni bora za kilimo cha zao hilo utapata pesa ambayo hujawahi kuipata” alisema Mwanri.
“Kijana uliyekuja hapa leo ninakuambia kuwa kama unarafiki yako unashinda nae kijiweni na kucheza karata, Pool kuanzia leo achana naye …kwani hana nia njema nawe…mwambie kuwa Mkuu wa Mkoa amenifundisha juu ya kulima pamba kisasa kuanzia sasa urafiki wangu mimi na wewe bye bye” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Alisema kuwa urafiki usio kuzungumzia mashindani katika kufanya kazi za maendeleo haufai na vema vijana wakazungumzia zaidi ya kujiletea maendeleo na sio kushinda vijiweni huku wakiendelea kuishi katika hali ya kutaka kuendelea kukumbatia umaskini.
kukaa kijiweni kuendelea kusikiliza maeneo yasiyo na maana hayawezi kuwasaidia vijana kuwaletea mandeleo bali yataendelea kuwafanya kuwa maskini.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa elimu aliyoitoa katika maeneo mbalimbali juu ya kulima pamba kisasa na kuzingatia Sheria za zao hilo.
Alisema kuwa kitendo cha yeye kukubali elimu ya kilimo cha zao hilo huku mvua ikimunyeshea ni ishara tosha kuwa amekusudia kuwawekea kazi wa Tabora mazingira wezeshi ili kuondokana na kilimo kisicho na tija na akisaidi kuinua maisha yao.
Kasele alisema kuwa wao Uongozi wa Halmashauri ya Kaliua wameanza kupambana na wazurulaji wakati wa msimu ya kilimo kwa kuwakata watu wote wanaoshinda vijiwe ikiwemo vya kahawa badala ya kwenda mashambani kulima.
Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa kila mtu mwenye uwezo wa kufanyakazi anakwenda shamba kulima na sio kushinda katika vijiwe vya kahawa bila jambo la msingi.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama alisema kuwa yeye na Maafisa Wengine watahakikisha wanakwenda katika maeneo ya vijijini kuwasimamia wakulima ili waweze kulima mazao yote kitaalamu na kwa kuzingatia kanuni za kilimo bora.
Alisema kuwa lengo ni kutaka Wilaya hiyo inaongoza katika uzalishaji wa mazao yote ikiwemo pamba ili kuboresha maisha ya wakulima na kuongeza mapato ya Halmashauri.
Mkuu wa Tabora yuko katika ziara mkoani mwake kuhamasisha kilimo cha kisasa cha zao la pamba na mazao mengine ikiwa ni sehemu kutaka wakulima pesa zitakazoboresha maisha yao.

0 Comments