Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu (kushoto)akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, wakati wa kuwatambulisha Bondia Mtanzania Ibrahim Mgendera(Katikati) anayetarajia kutetea ubingwa wake wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight dhidi ya bondia kutoka Afrika ya Kusini KOOS SIPHO SIBIYA(hayupo pichani) Pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa limedhaminiwa na Vodacom Tanzania na Azam TV na litafanyika jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam,Kulia ni Mkuzaji wa Vipaji vya ngumi Tanzania ,Joe Anea.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akishuhudia mabondia Ibrahim Mgendera kutoka Tanzania na kocha wake (wapili kushoto)na bondia kutoka nchini Afrika Kusini,KOOS SIPHO SIBIYA na kocha wake(wapili kulia)wakitambulishwa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa mkutano na waandishi hao uliofanyika Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa limedhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC, AzamTV litafanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,Katikati ni mwamuzi wa mpambano huo wa Kimataifa kutoka nchini Ujerumani, Arno Pokrandt.
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Bondia Mtanzania Ibrahim Class Mgendera, anatarajia kutetea ubingwa anaoushikilia
wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC)
uzito wa “Lightweight dhidi ya bondia kutoka nchini Afrika Kusini
Pambano hilo
la kimataifa la ngumi za kulipwa ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya
Vodacom PLC pamoja na kampuni ya Azam, litafanyika jijini Dar es Salaam Novemba
25 2017 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mgendera anashikilia ubingwa wa mkanda wa dunia wa
Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight”ambao
alioutwaa nchini Ujerumani tarehe 1 Julai, 2017 kwa kumpiga Jose Forero wa
Panama. Bondia huyo atakuwa ni kibarua kigumu cha kutetea taji hilo mbelea ya KOOS SIPHO SIBIYA kutoka AFRIKA YA KUSINI
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi,Yusuph Singo alisema maandalizi ya pambano hili yalianza siku tarehe
5 August siku ya hafla ya kumpongeza
bingwa huyo ambapo mgeni alikuwa ni
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe ambapo
Uongozi wa bondia hiyo ilimwelezea
Waziri mwenye dhamana na michezo kwamba, mkanda huo unapaswa kutetewa katika
kipindi cha miezi mitatu tangu alipoupata na tayari kulikuwa na ofa mezani za
kuutetea mkanda huo kutoka katika nchi za Marekani, Ujerumani na Ufilipino.
“Mheshimiwa alisikiliza hoja hizo na kuweza
kuzifanyia kazi kwa kuwatafuta wadhamini na wadau wa michezo nchini ili
kuwezesha pambano la kutetea mkanda huo lifanyike hapa nyumbani kwa kuhamasisha
mchezo wa ngumi za kulipwa pamoja na kuwapa burudani mashabiki wa mchezo huo
hapa nchini,alisema Singo
Nikiwa kama mwenyekiti wa maandalizi ninapenda
kutoa shukurani zetu za dhati kabisa kwaniaba ya mheshimiwa waziri kwa
Wadhamini wakuu wa masumbwi haya AZAM pamoja na Vodacom Tanzania PLC,kamati ya
pamoja ya kufanikisha pambano hilo ikijumuisha Baraza la Michezo la Taifa,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Menejimenti ya Joe’s Gym na
Kamishei ya Ngumi za Kulipwa Tanzania.
Akizungumzia kuhusu udhamini wao, Meneja Uhusiano wa
Vodacom Tanzania PLC,Matina Nkurlu alisema kampuni yao imeamua kutoa udhamini
ikiwa kama ni sehemu yake katika kuendeleza na kukuza mchezo wa ngumi
“Vodacom imekuwa ikiendeleza na kudhamini michezo mbali mbali hapa nchini ikiwamo soka ambapo
sisi ndiyo wadhamini wakuu wa Ligi ya Tanzania bara(VPL). Udhamini wetu hauishi
tu kwenye soka bali kwenye michezo mingine mingi tunapenda kutoa wito kwa
watanzania kujitokeza kwa wingi na vilevile tutawawekea na bidhaa mbalimbali
ukumbini hapo na watazipata kwa bei nafuu kabisa na pia tutatoa elimu kwao
kuhusiana na kifurushi chetu kilichopo sokoni kwa sasa cha Pinduapindua,”
alisema Nkurlu
Bondia atakayepambana na Mgendera anatarajia
kuwasili nchini tarehe 22 Novemba, 2017. Pambano hilo litanogeshwa na mapambano ya utangulizi ya
kimataifa likiwakutanisha mabondia kutoka Tanzania na Malawi, mabondia wanawake
pamoja na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii nguli wa muziki wa kizazi
kipya.

0 Comments