Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa
Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa akimtambulisha Mgombea Udiwani Kata ya
Chipogoro Hosea Fweda.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa
Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa na Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde wakimtambulisha Mgombea Udiwani Kata ya
Chipogoro Hosea Fweda kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa
Kamati kuu ya CCM Alhaj Adam Kimbisa akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya
Chipogoro .
Mbunge wa
Jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akitoa somo kwa vijana na wananchi wa
kata ya Chipogoro wakati uzinduzi wa kampeni za udiwani.
Mbunge
wa jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akionyesha ujuzi wake wa kucheza
ngoma za kigogo wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani Kata ya
Chipogoro.
.........
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa
Dodoma kimezindua kampeni kwa kishindo kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa udiwani
katika kata ya Chipogoro huku kikiwataka wakazi wa kata hiyo kuendeleza heshima
iliyopo ya Dodoma kuwa ngome ya CCM.
Katika uzinduzi huo kimepokea kadi za Chama Cha ACT
Wazalendo mia nane ikiwemo kadi ya aliyekuwa katibu wa chama hicho mkoa wa
Dodoma Weston Kaduma.
Akizindua kampeni hiyo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma
alhaj Adam Kimbisa amesema siku zote Dodoma ni ya CCM hivyo watumie uchaguzi
huo kumpa rais nguvu kwa kumchagua Hosea Fweda na kutoiyumbisha CCM.
“Juzi kuna chama kilikuja kuzindua kampeni zake hapa,kuna
vijana walienda,nawapongeza vijana wale kwa kwenda kuwapa kampani lakini nina
uhakika ndani ya mioyo yao wanasema wataipigia kura CCM, maana ndugu zangu
mgeni akija kwako ukimuacha peke yake hatojisikia vizuri,”amesema
Kimbisa.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mbunge wa Mtera
Livingstone Lusinde aliwataka wakazi wa Chipogoro kuimarisha umoja wao,kuepuka
vurugu,kushauriana,kubishana kwa hoja na kumchagua diwani anayetokana na CCM
ambaye ni Hosea Fweda.
“Ndugu zanguni mchagueni Hosea atetee shida
zenu,awasilishe shida zenu kwa tajiri,sasa ukimchagua Jafari anapeleka wapi
shida zenu kwa Mbowe?Mbowe apelekewe ana serikali?lakini ukimchagua Hosea awe
diwani wa Kata hii kwa tiketi ya CCM atapiga mpira utapokelewa na mbunge,mbunge
nae atapiga shuti kali mpaka golini ambapo ni kwa rais,”alisema Lusinde.
Kwa upande wake mgombea Fweda amewaomba wananchi wamchague
ili ashirikiane nao katika kuwaletea maendeleo na kuahidi kuwa diwani wa
Chipogoro katika kuwatumikia.
“Nichagueni mimi najua changamoto zilizopo katika kata hii
ikiwemo ukosefu wa umeme,kituo cha afya na kwamba kwa kutumia viongozi na
serikali ya CCM changamoto hizo tutazitatua,”alisema Fweda.
Mkoa wa Dodoma unafanya uchaguzi mdogo wa marudio katika
kata moja ambayo ni ya Chipogoro.





0 Comments