Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii Bibi. Sihaba Nkinga katika Mkutano wa wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii unaomalizika leo Mjini Dodoma na kuwasisitiza kwenda kuleta
mabadiliko sehemu walizopo.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
...
Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.
Sihaba Nkinga amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kwenda kuleta
mabadiliko katika maeneo yao.
Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati wa Siku ya mwisho ya
Mkutano wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo unaomalizika leo mjini Dodoma na
kusisitiza kuwa wao ni watu muhimu na wanayodhamana ya kuleta mabadiliko katika
maeneo yao kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo
jumuishi na endelevu.
Ameongeza kuwa ubunifu na uwajibikaji kwa Afisa
Maendeleo ya Jamii ni tunu kubwa itakayowezesha wawezesha kuwa chachu ya
mabadiliko katika maeneo
mnayotumika jamii.
“Niwaombe Maafisa Maendeleo ya Jamii mliopo hapa na muwafikishie
ujumbe wasiokuwepo katika Mkutano huu kuwa wanatakiwa kuwa chachu ya mabadiliko
katika maeneo yao” alisema Bibi. Sihaba.
Aidha, Bibi Sihaba Nkinga amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii
kama wasajili wasaidizi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Serikali kuwajibu wa
kuonesha uzalendo na utanzania wetu kwa kuhakikisha kuwa mashirika (NGOs)
yanafanya kazi kwa kuzingatia Sheria, taratibu na Kanuni ili kutoa mchango
katika sekta zinazosisimua ukuaji wa maendeleo ya nchi na kusisimua ustawi wa
jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
Bw. Marcel Katemba amewashauri Maafisa Maendeleo ya Jamii kuzingatia Kanuni na
Sheria katika kuratibu ufanyaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika
maeneo yao.
“Tuzingatie Sheria na Kanuni katika kuyaratibu Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali katika maeneo yetu” alisema Bw. Katemba
Naye kwa niaba ya Maafisa Maendeleo ya Jamii Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kyela Bi. Nelusigwa
Mwakigonja ameishukuru Wizara mama kwa kuwaleta pamoja Maafisa Maendeleo ya
Jamii na kutoa maelekezo kwao ili waweze kuleta mabadiliko katika sehemu zao za
kazi.
“Tunaishukuru Wizara kwa kutuleta pamoja na tunaahidi
tutaenda kuyatekeleza maelekezo yote tuliyoyapata kutoka kwa viongozi wetu”
alisema Bi Nelusigwa.

0 Comments