Mwenyeketi
wa kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Mhe. Peter Serukamba.
.....
Na.WAMJW.Dodoma
Taasisi ya Chakula na lishe nchini imetakiwa kujikita katika
kutoa elimu kwa umma ili wananchi waweze kujua faida ya kula chakula bora na
kuepukana na utapiamlo na udumavu
Hayo yamesemwa na Mwenyeketi wa kamati ya Bunge ya huduma na
maendeleo ya jamii Mhe. Peter Serukamba
wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utendaji wa shughuli za taasisi hiyo mjini
Dodoma leo.
Mhe.Serukamba alisema bila elimu kwa umma wananchi watakuwa
wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya matibabu kwa kuwa hali ya udumavu ni mkubwa
,?watu wakiwa na chakula na lishe bora unakuwa na uhakika hutougua hovyo na
kupoteza fedha nyingi kwa ajili ya matibabu,lakini wakijua wale mlo gani ambao
ni sahihi hii itasaidia kutokomeza kabisa tatizo hili?
Aidha, alisema Tanzania haina tatizo la chakula ila
hawafahamu ni mlo gani sahihi wanapaswa kula hivyo kwa kutoa zaidi elimu itakua
ni kinga na itasaidia wananchi wasiugue
?Taasisi hii iboreshwe na mkishirikiana na Tamisemi,wakulima
na wasafirishaji wa mazao kupitia maofisa maendeleo ya jamii mtawafikia
wananchi wengi na hakutokuwa na vizazi vyenye udumavu na matatizo ya akili.
Awali akiwasilisha taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo Naibu
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto dkt.Faustine Ndugulile
alisema zaidi ya asilimia 35 ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano nchini vinachangiwa na matatizo ya lishe duni na katika kipindi cha mwaka 199 hadi 2015/2016
vifo vya watoto vimepungua kutoka 147
hadi 67 kwa kila vizazi hai 1000.
?Serikali inafanya jitihada kubwa katika kumjenga mtoto ili akue vizuri kimwili
na kiakili kuanzia siku elfu moja za mwanzo za mtoto ambazo ni muhimu kwa
makuzi ya mtoto?.
Hata hivyo dkt.Ndugulile alisema hali ya lishe nchini
inaendelea kuimarika kutokana na kupungua kwa viwango vya utapiamlo nchini kati
ya mwaka 1992 na 2015.
Alisema udumavu (urefu wa umri) umepungua kutoka asilimia
49.7 hadi 34.4 na mikoa inayoongoza ni Rukwa (56%) na Ruvuma (44%) ,kwa upande
wa ukondefu (uzito kwa urefu) kutoka asilimia 7.8 hadi 4.5 na mikoa inayoongoza
ni Zanzibar-Kusini Pemba na Kaskazini Pemba(9%),Manyara (6.4%),Geita
(6.2%),Kigoma (6%) na Morogoro (6.0%)
Kwa upande wa uzito pungufu alisema (uzito kwa umri) kutoka
asilimia 25.1 hadi 13.7 na mikoa inayoongoza ni Rukwa (23%),Arusha (20%) pamoja
na Kigoma (20%).
Vilevile,mwanamke mmoja kati ya kila wanawake 10 walio
katika umri wa kuzaa ana uzito pungufu (underweight) wakati asilimia 18 wana
uzito mkubwa (over weight) na asilimia 10 wana kiribatumbo(obesity).Mikoa
inayoongoza kwa kiribatumbo ni Zanzibar mjini Magharibi kwa 22%,Unguja Kusini
19%,Dar es Salaam 21%,Kilimanjaro 19% na Tanga 17%.
Naibu Waziri huyo aliahidi kuwa watajipanga katika kutoa
elimu ya afya kwa umma na kuwafikia wananchi wengi zaidi ?bado Watanzania
hawajui kula lishe iliyokamilika na matumizi bora ya chakula.

0 Comments