Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo akizungumza na wananchi wa kata ya Engusero –Wilayani Kiteto wakati wa
ziara yake ya kazi Wilayani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo (katikati) akimskiliza Meneja wa TARURA Wilaya ya Kiteto Eng.Gerald
Matindi akielezea hali ya ujenzi wa barabara ya Namelock-Sunya.a
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo(kwanza kushoto) akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto
Mhe. Tumaini Magesa, Mbunge wa Kiteto Mhe.Emanuel Papiyani na Mwenyekiti
wa Ccm Wilaya wakikagua ujenzi wa barabara ya Namelock –Sunya eneo linalojengwa
na Mkandarasi Maginga Business Holdings Company Ltd ya mjini Dodoma.
Muonekano wa barabara ya Namelock –Sunya eneo linalojengwa na
Mkandarasi Maginga Business Holdings Company Ltd ya mjini Dodoma ambaye yuko
site kwa miezi minne sasa lakini hali ya ujenzi wa barabara hiyo ikiwa
hairidhishi.
Nteghenjwa hosseah, Kiteto
Kampuni ya Maginga Constraction ya mjini Dodoma iliyopewa
kandarasi ya ujenzi wa barabara ya Namelock – Loltepes-Sunya Wilayani Kiteto
kwa kiwango cha lami imekwamisha mradi huo kwa kutofanya kazi zilizoainishwa
kwenye mkataba kwa kipindi cha miezi minne baada ya kukabidhiwa kazi hiyo.
Akikagua barabara hiyo wakati wa ziara ya kikazi Wilayani humo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo ametoa siku kumi na nne kwa Mkandarasi huyo kukamilisha kazi au
kurejesha kazi hiyo kwa Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA)
ili apewe Mkandarasi mwingine atakayeweza kwenda na muda uliyoainishwa
kwenye mkataba.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Waziri Jafo amesema tar
17/10/2017 nitakuja tena hapa kuangalia maendeleo ya mradi huu; Mkandarasi huyu
afanyiwe tathmini ya haraka kama ana uwezo wa kufanya kazi hii ama lah
msitishe mkataba wake kwa sababu mpaka sasa hivi amekwishatumia nusu ya muda
aliyopewa lakini alichofanya hakielewi na barabara hii ni muhimu kwa matumizi
ya wananchi haswa wakulima ambao hutumia barabara hii kusafirisha mazao yao
toka shambani hadi Sokoni.
“Siwezi kuvumilia wananchi wangu wapate tabu kwa sababu ya uzembe
wa mkandarasi ninaagiza mambo matatu, Mkandarasi aondolewe haraka na apatiwe
atakayeweza kufanya hii kazi ama kazi zilizoainishwa kufanyaika katika
kipindi cha miezi mine zionekane zikiwa kwenye ubora au tumuondoe Meneja wa
Tarura Wilaya ya Kiteto na tumlete atakayeweza kusimamia miradi kwa
ufanisi”aliongeza Mhe.Jaffo.
Akielezea hali ya mradi Mbunge wa Kiteto Mhe.Emanuel Papian
amesema haridhishwi na utendaji kazi wa mkandarasi Maginga Hoding Cooperation
kutokana na uzembe anauofanya kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya
Namelock-Sunya yenye urefu wa Km 44 na amekwisha mlalamikia mara kadhaa kwenye
uongozi wa Wilaya pamoja na TARURA lakini haoni hatua stahiki zikichukuliwa
dhidi yake.
“Mradi huu walipewa wakandarasi wawili mmoja akiwa huyu Maginga
ambaye anatakiwa kujenga barabara ya urefu wa Km 44 ambaye anajenga kuanzia
namelock mpaka Loltepes ambae namlalamikia leo hii na Mkandarasi mwingine
ni Deniko Constraction ambaye naye anajenga Km 44 kuanzia Loltepes mpaka
Sunya lakini yeye ameshafanya kazi kubwa na yenye ubora; Sasa nashangaa kwanini
huyu Maginga yeye hafanyi na hachukuliwi hatua yeyote ninaomba Mhe.Waziri
uingilie kati suala hili” alisema Mhe.Papian.
Naye Meneja wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Gerald Matindi
amesema changamoto hiyo walikwishaibaini na kumuandikia Mkandarasi Maginga
barua ya kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na wanaendelea na
kufuatilia na endapo watathibitisha hawezi kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo
watasistisha mkataba wake mara moja.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Namelock – Loltepes-Sunya
inajengwa kwa urefu wa Km 88 ambapo wakarasi wawili Maginda constraction pamoja
na Deniko Constractio wamepewa kazi ya kujenga kila Km 44 kila mmoja na kazi
zilizoainsha ni pamoja na ujenzi wa madaraja, makalavat, mifereji ya kusafirishia
maji ya mvua pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe.
Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi March,2018 na itagharimu
Fedha za kitanzania zaidi ya shilingi Bil 7 ambazo ni Fedha za ruzuku “Feed for
Future” ikiwa ni msaada kutoka katika Serikali ya Watu wa Marekani “USAID:
Fedha hizi hujenga barabara kwenye halmashauri zenye mazao mengi ili
kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka shambani hadi Sokoni.




0 Comments