Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maafisa wa
Uhifadhi wa Wanyamapori wamefanikiwa kumkamata jangili akiwa na meno ya
Tembo 5 yenye thamani ya MIL 100 name mshitakiwa yuko kituo cha Polisi
morogoro.
Taarifa kutoka kwa jeshi la Polisi morogoro mshtakiwa
anategemea kufikishwa mahakamani. Aidha, Afisa Habari wa Mamlaka ya
Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA Bw. Twaha Twaibu ameeleza kuwa
walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa jangili huyo wa
meno na kutuma maafisa wanyamapori kutoka Makao Makuu ya TAWA
wakishirikiana na jeshi la Polisi na kuweza kumkamata jangili huyo.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei
akiongelea tukio hilo, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo
aliejulikana kwa jina la Nehemiah Nashon akiwa katika chumba namba 104
cha Hoteli ya BZ iliyopo maeneo ya Nane-nane Mjini Morogoro, na kwamba
vipande hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 100.
Jangili sugu akiwa na shehena ya meno ya tembo akiwa chini ya ulinzi mkali.




0 Comments