Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishikana
mkono na kupongezana na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo
toka Hoima nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani Tanga. Sherehe za
uwekaji wa jiwe hilo zimefanyika katika eneo la Mutukula Wilayani Kyotera
nchini Uganda
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji
wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maelezo ya namna ya
bomba hilo la mafuta ghafi litakavyojengwa na kuanza kufanyakazi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji
wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta wakijadiliana jambo mara baada ya kupewa
maelezo ya mradi huo mkubwa wa bomba la mafuta ghafi.
Jiwe
hilo la Ufunguzi la Ujenzi wa Bomba hilo la Mafuta ghafi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji
wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiondoka katika eneo la Mutukula
mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la bomba la mafuta.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama
Janeth Museveni katika eneo la mpaka wa Tanzania Mutukula kabla ya ufunguzi wa
Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania na Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni
wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili upande wa
Tanzania kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande
wa Tanzania na Uganda.
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasili pamoja na Mke wa Rais wa Uganda Mama
Janeth Museveni wakiangalia ngoma katika eneo la Mutukula upande wa Uganda.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke
wake Mama Janeth Magufuli wakifurahia ngoma za asili za watoto wa Uganda mara baada ya kuwasili
nchini humo huku Rais wa Uganda Yoweri Musevini akitazama watoto hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wa nyimbo za mataifa ya Tanzania na Uganda zikipigwa katika eneo la Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakifungua Ofisi za
Kituo cha pamoja cha huduma za mpakani kwa upande wa Tanzania. Wanne kutoka
kushoto ni Mke wa wa Rais Mama Janeth
Magufuli akishuhudia pamoja na Mke wa Rais Museveni Mama Janeth Museveni wa
kwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakizungumza na mamia ya wananchi hawaonekani pichani katika eneo la Kyatera nchini Uganda mara baada ya ufunguzi wa Bomba la Mafuta.
PICHA NA IKULU














0 Comments