Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa amewasili katika Viwanja vya Kili
Golf Jumapili Mkoani Arusha kwa ajili ya
kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf Kulia ni Katibu Wake Bw.
Andrew Magombana na kushoto ni Bw. Chris Martin Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf
Tanzania(Tanzania Golf Union).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kili Golf Bw. Bastiaan Bruins (Kushoto) baada ya kuwasili katika viwanja hivyo
kwa ajili ya kufunga mashindano ya Wazi
ya Tanzania Kili Golf katikati ni Makamu
wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union) Bw. Chris Martin.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na waandaji wa mashindano ya Wazi ya Kili Golf Mkoani Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa
risala kwa washiriki wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katika halfa
ya kufunga mashindano hayo jana Mkoani Arusha.
Mshiriki kutoka Kenya Bw. Edwin Mudanyi akijiandaa kupiga mpira wakati wa fainali wa
mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha ambapo jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Kenya,
Uganda, Malawi, Zambia, Afrika ya Kusini na Tanzania walishiriki.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpa
mkono wa hongera mmoja wa washindi wa kwanza Bw. Victor Joseph kutoka Tanzania
baada ya kumalizika kwa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani
Arusha.
(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).
..
Na
Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.
Serikali imeahidi
kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa mchezo wa Golf nchini katika kuhakikisha
mchezo huo unafundishwa kuanzia ngazi ya chini ili kuandaa wachezaji bora wa
kimataifa wataoiwakilisha nchi katika mashindano hayo duniani.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe alipokuwa akifunga mashindano ya
Kili Golf Mkoani Arusha ambapo ameeleza kuwa mchezo huo ni wa muhimu ukazingatiwa katika kukuza sekta ya michezo.
“Mchezo huu wa Golf
ni mzuri sana kwa kuwa unakusanya watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaleta
pamoja nami naahidi kuwa Wizara yangu itahakikisha inashirikiana kwa karibu na
wadau wa Golf nchini ili kuukuza zaidi” amesema Mhe. Dkt. Mwakyembe.
Mhe. Dkt. Mwakyembe
ameongoza kwa kuwataka washiriki wa mchezo huo kuwa mabalozi wazuri katika
kuutangaza mchezo huo ndani na nje ya nchi na kuhamasisha vijana wengine kuwa
na moyo wa kujifunza.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa Kili Golf Arusha Bw.Bastiaan Bruins amesema kuwa lengo la
mashindano hayo ni kuhakikisha mchezo huo unafahamika kwa watu wengi na kuondoa
dhana iliyojengeka kuwa ni mchezo wa kitajiri.
“Mashindano haya ni
kuwapa hamasa watanzania kuupenda,kujifunza na kuelewa mchezo huu wa Golf ambao
ni mchezo rahisi sana na unachangamasha akili huku ukiwaleta watu kutoka sehemu
mbalimbali kuwa kitu kimoja” amesema Bw.Bruins.
Kwa upande wa washiriki wa mashindano hayo hususani
kutoka nje ya Tanzania wamewashukuru waandaaji na watanzania kwa ukarimu,
upendo,ushirikiano na umoja
waliouonyesha huku wakiahidi kushiriki tena mashindano mwakani.
Mashindano ya Wazi ya
Kili Golf Tanzania yalifunguliwa rasmi Novemba 10 mwaka huu yakiwa na jumla ya
washiriki 250 kutoka nchi za Malawi,Zambia, Afrika ya Kusini, Uganda , Kenya na
wenyeji wao Tanzania huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na washindi wawili
baada ya kutoka sare katika mchezo wa mwisho ambao ni Bw. Edwin Mudanyi kutoka
Kenya na Bw. Victor Joseph kutoka Tanzania.
0 Comments