Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Cheti cha Mfumo wa Uhakiki Ubora wa Huduma cha Kiwango cha Kimataifa
(ISO 9001:2015) Jijini Dar es Salaam. TFDA imekuwa ya kwanza
miongoni mwa mamlaka zinazoshughulika na udhibiti wa ubora wa chakula na
dawa katika ukanda wa Afrika Masharika kutunikiwa cheti hicho.
Picha
ya pamoja ya meza kuu ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Faustine Ndugulile wakiwa wameshishika cheti cha mfumo wa Uhakiki Bora katika
Kiwango cha Kimataifa Cha Iso 9001-2015.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelekezo mbele
ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo wakatikati na Mwenyekiti wa Bodi
ya TFDA Dkt Ben Moses.
Picha
ya pamoja ikiongozwa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wakati akizindua CHETI CHA MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA
KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 tukio lililofanyika katika viunga vya
Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Meneja Uchunguzi wa Dawa na Vipodozi
Dkt. Yonah Hebron akitoa maelekezo mbele ya Naibu Waziri Dkt. Faustine
Ndugulile wakati akitembelea maabara katika viunga vya Mamlaka hiyo jijini Dar
es Salaam, kulia kwa Naibu Waziri ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula,
Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakwanza kushoto
akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu TFDA wapili,
Mwenyekiti wa Bodi ya TFDA Dkt. Ben Moses wa tatu, na wa mwisho ni
Meneja uchunguzi wa chakula Dkt. Mziray
NA
WAMJW-DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Chakula , Dawa na Vipodozi TFDA imetakiwa
kuboresha udhibiti wa uingizaji wa Dawa,
Vipodozi na Chakula nchini kiholela ili
kulinda afya ya Watanzania .
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kuzindua CHETI CHA
MFUMO WA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA KATIKA KIWANGO CHA KIMATAIFA CHA ISO 9001-2015 jijini Dar es Salaam.
“Dawa ni kitu nyeti sana, hatuwezi kuruhusu dawa
feki kuingia nchini, mnafanya kazi nzuri sana katika nyanja hii na muendelee na mpango huu ili kudhibiti
uingizaji wa vyakula visivyokidhi viwango na mahitaji ya watanzania, ” alisema
Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa TFDA wanatakiwa
kuzingatia muongozo wa kupitisha vyakula na vipodozi kwenye mipaka ya nchi kwa
kuzingatia ubora na viwango vilivyoweka katika kudhibiti uingizaji mbovu wa
vyakula.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti
Silo amesema kuwa ili kuendelea kukidhi matakwa ya wateja na mahitaji yao
wameamua kuendana na kiwango cha kimataifa na kuwaita ISO kuja kuhakiki ambapo
wamefanikiwa kukidhi na kupata cheti.
“Shirika la Viwango la Kimataifa ISO limehakiki
ubora wa huduma zetu katika kukidhi mahitaji na matakwa ya watumiaji wa huduma
zetu na kutupatia cheti kinachoturuhusu kutoa huduma nchini” alisema Bw. Silo.
Aidha Bw. Silo amesema kuwa wapo bega kwa bega na
Serikali ya awamu ya tano ianyoongozwa na Rais Dkt. John pombe Magufuli katika
kusogeza mbele gurudumu la afya hapa nchini kupitia taasisi ya TFDA.









0 Comments